... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Yote Yanaanzia Moyoni

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mithali 27:19 Kama uso ufananavyo na uso katika maji; kadhalika moyo wa mtu humwonyesha alivyo.

Listen to the radio broadcast of

Yote Yanaanzia Moyoni


Download audio file

Kuna jambo moja muhimu katika maisha ya mwanadamu kuliko yote, Nalo ni hili:  lazima mtu awe mkweli akijikagua,  Kujihoji na kujiona kama tulivyo hadi sasa.

Haujambo?  Mimi ni Berni Dymet ninakukaribisha kwenye hiki cha NENO SAFI NA LENYE AFYA.    

Uwezo wa kujitathimini na kutathmini mazingira yetu pamoja na mwitikio wetu kwa mambo kadhaa wa kadhaa, kwa kweli ni kipawa kinachotoka kwa Mungu mwenyewe.  Hakuna kiumbe kingine hapa duniani awezaye kujihoji kama mwanadamu.

Lakini mara nyingi, ni kipawa tunachokipuuza, tukiishi kila siku kama kawaida, tukilala na kuamke alafu asubuhi tunayarudia mambo  yale yale.

Kila asubuhi tunajiangalia kwenye kioo.  Lakini ni lini twaweza kutulia na kutafakari kinachoendelea mioyoni mwetu?  Kwa nini moyo wangu uko hivi?  Je!  Ningewezaje kuishi tofauti na kuwa na mwitikio ulio bora kuanzia leo?  Hmm?

Mithali 27:19  Kama uso ufananavyo na uso katika maji; kadhalika moyo wa mtu humwonyesha alivyo.

Kuna hatari wakati mtu anapambana na maisha ya kila siku. Miaka nenda rudi hadi sasa imekuwa ni tabia sugu.  Lakini tukumbuke kwamba yote tunayofanya na tabia yetu … yote yanaanzia moyoni.

Moyo wa mtu humwonyesha alivyo.

Sasa, niambie.  Je!  Wewe ni mtu wa namna gani?  Umebadilika kuwa mtu wa namna gani?  Je!  Hivyo ndivyo unavyotaka uwe?  Je!  Hivyo ndivyo unavyotaka kuishi?  Yatafakari maswala hayo.  

Moyo wa mtu humwonyesha alivyo.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.