... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Usiwe Mwenye Aibu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Warumi 1:16 Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia.

Listen to the radio broadcast of

Usiwe Mwenye Aibu


Download audio file

Kwa kawaida kujiona wa fahari si jambo jema, tunapojaa kiburi na kunia makuu huwa haipendezi, si kweli?  Mungu anapinga wenye kiburi japo kuona fahari ni jambo jema wakati mwingine.

Kama vile mzazi yoyote; mimi nami ninaona fahari leo watoto wangu ni watu wazima, niliona fahari namna walivyokuwa wakikua na kukomaa, inafurahisha sana, kwani ni vibaya kuona fahari kwa jambo kama hilo!?  Sidhani.  Fahari inaweza kugeuka kuwa kiburi ikilenga mtu mwenyewe, yaani ile hali ya mtu kujiona kuwa bora badala ya kuonea fahari wengine.

Sisemi kwa kulenga watu tu, hapana, hata Mungu pia, Kwa sababu; nikichunguza mazingira naona watu wengi sana wanaojiita Wakristo lakini hawamuonei fahari Kristo, wanamuogopa na kumuonea aibu Mwokozi aliyetoa uhai wake kwa ajili yao. Lakini Mtume Paulo hakuogopa: 

Warumi 1:16  Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia. 

Kama tunakiri kwamba tunamwamini Yesu, tusimwonee aibu, Ni kweli, kuna watu baadhi watakushutumu ukimtetea Kristo, lakini kama vile Pat Steele alivyosema:  Msiba wa kuona watu wanakwenda Jehanamu milele unanigusa zaidi ya namna ambavyo watu wanavyonipenda wakati huu.  Mimi ni mfuasi wa Yesu na siionei haya Injili kwasababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu kwa kila aaminiye. 

Usiionee haya Habari Njema ya Yesu.   Uhai wa mtu unategemea kusikia habari hiyo. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.