... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Je!, Unanung’unika Kiasi Gani?

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Wakorintho 10:10,11 Wala msinung’unike, kama wengine wao walivyonung’unika, wakaharibiwa na mharabu. Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani.

Listen to the radio broadcast of

Je!, Unanung’unika Kiasi Gani?


Download audio file

Hakuna ubaya kama mtu anayenung’unika kila siku, Mtu anayenung’unikia kila jambo; kana kwamba dunia nzima ni mdaiwa wake.  Kwake hakuna yaliyo bora wala hakuna mtu anayefaa.  Kwa ujumla kwake maisha yananuka tu.

Je!, Unapenda kuwa karibu na mnung’unikaji wa namna hiyo?  Ukimuona tu anakujia, basi unajaribu kumkwepa kwa kuhama njia, sindiyo?  Ni kweli.  Watu wenye tabia ya kunung’unika hawapendezi kabisa.

Sawa. Sasa jaribu kwanza kuangalia swala hili kwa mtazamo wakiMungu. Yeye anajua kila kitu tunachokifanya.  Sasa tunapo nung’unika kwa ndani au kwa kutumia sauti,…haijalishi, Mungu anafahamu yote.

Sasa, je, atafurahia kiasi gani kusikia manung’uniko yetu?  Akiongea habari ya Waisraeli kutoka Misri wakielekea Nchi ya Ahadi, alikuwa na maneno ya kuwalaumu:

1 Wakorintho 10:10,11  Wala msinung’unike, kama wengine wao walivyonung’unika, wakaharibiwa na mharabu.  Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani.

Mtu akisoma maneno hayo, ataona kwamba Mungu anachukizwa na manung’uniko yetu.  Ni kashfa.  Lazima wewe na mimi tusikie onyo hili kali.  Kunung’unika kunaua.  Kunatafuna nafsi ya mtu kama kansa.

Kwa vyovyote, ingekuwa bora kabisa, tena ingetupa uwezo wa kubadilika kama tungempelekea Mungu dua na maombi juu ya matatizo yetu badala ya kunung’unika.

Wala msinung’unike, kama wengine wao walivyonung’unika, wakaharibiwa na mharabu.    

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.