... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Je! Utaafikiana na Uovu?

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Kumbukumbu 6:4,5 Sikiliza, Ee Israeli; BWANA, Mungu wetu, BWANA ndiye mmoja. Nawe mpende BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote.

Listen to the radio broadcast of

Je! Utaafikiana na Uovu?


Download audio file

Kuna wakati tunajikuta katika kitendawili cha maadili.  Kwa upande mmoja, mtu anafahamu yaliyo mema na kwenye kiini cha moyo wake anataka kutenda haki.  Lakini ushawishi wa mafanikio ya muda mfupi yanayotokana na kutenda visivyo ni mkubwa kiasi cha kutuvuta sana.  Kama ingekuwa wewe, ungeelekea upande gani?

Zamani miaka ile ya 1980, wanajeshi wenzangu wawili, baada ya sisi kutoka jeshini, tuliunda kampuni ya ushauri wa teknolojia.  Graham alitoka jeshini akiwa Kanali, Marko akiwa Meja na mimi Kapteni tu.  Sasa kwa kuwa Graham alitupita cheo na kwa kuwa alikuwa na akili kuliko sisi, tulimfanya kuwa bosi.  Alikuwa mtu wa imani kabisa na bado yuko hivyo.  Lakini mimi, wakati ule, sikuwa na imani kabisa.

Tangu mwanzo, aliweka kanuni itakayotungoza – kwamba, haijalishi ingetugharimu nini, daima tungetoa ushauri bora kwa wateja wetu, na si kwa faida yetu.   Na hii ilikuwa sahihi

Hatimaye, kwa sababu ya msimamo wetu huo, tulipata sifa njema kwa wateja kwamba tu watu waadilifu na hii ilisababisha tupate kazi nyingi sana kuliko tulivyokuwa tumetarajia.  Kama vile mteja wetu mmoja alivyoniambia siku moja, “Unajua, mayai, daima yanaelea juu kutoka ndani ya maziwa.”

Ni yupi unayomfanya kuwa wa kwanza maishani mwako?  Ni kwa ajili ya nani au kwa ajili ya nini huwezi kubisa kuafikiana na yasiyo haki, hata kama mapato ya haraka-haraka yanayokushawishi?

Kumbukumbu 6:4,5  Sikiliza, Ee Israeli; BWANA, Mungu wetu, BWANA ndiye mmoja.  Nawe mpende BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote.

Usikubali kuanza kuuliza na kuweka “labda”, “walakini” au “pengine…”   Usikubali.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.