... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kuandaa Njia ya Bwana

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mariko 1:4-6 Yohana alitokea, akibatiza nyikani, na kuuhubiri ubatizo wa toba liletalo ondoleo la dhambi. Wakamwendea nchi yote ya Uyahudi, nao wa Yerusalemu wote, wakabatizwa katika mto Yordani, wakiziungama dhambi zao. Na Yohana alikuwa amevaa singa za ngamia na mshipi wa ngozi kiunoni mwake, akala nzige na asali ya mwitu.

Listen to the radio broadcast of

Kuandaa Njia ya Bwana


Download audio file

Mimi nimeshaona, kuna wakati Mungu anatenda mambo ya ajabu-ajabu. Yawezekana na wewe umeshashuhudia hayo.  Yaani mambo ambayo hatukuyatazamia kabisa, hadi tunajiuliza, ni Kwa nini?

Mfano, Yohana Mbatizaji, mtu aliyetumwa na Mungu atangulie mbele ya Yesu, kama vile Biblia inavyosema, kutengeneza njia ya Bwana.  Sawa.  Ni kweli, ilibidi njia iandaliwe.  Lakini huyu Yohana alikuwa mtu wa ajabu-ajabu:

Mariko 1:4-6  Yohana alitokea, akibatiza nyikani, na kuuhubiri ubatizo wa toba liletalo ondoleo la dhambi.  Wakamwendea nchi yote ya Uyahudi, nao wa Yerusalemu wote, wakabatizwa katika mto Yordani, wakiziungama dhambi zao.  Na Yohana alikuwa amevaa singa za ngamia na mshipi wa ngozi kiunoni mwake, akala nzige na asali ya mwitu.

Singa za ngamia, nzige, asali … ni mambo gani hayo?  Lakini hata kama alikuwa hivyo na akahudumia jangwani (si hekaluni wala katika sinagogi), bado watu walimwendea kwa wingi wasikilize mahubiri yake yaliyosumbua: badilisheni mienendo yenu; ili dhambi zenu zipate kusamehewa – maana yake, tubuni!

Si ujumbe wengi wanapenda kuusikia.  Tujiulize na sisi, je!  Ni ujumbe unaopenda kuusikia?  Lakini hata hivyo; walimwendea kwa wingi.  Ni kama Mungu katika hekima yake, alijua kwamba; watu walihitaji mabadiliko ya kina mioyoni mwao kabla ya kuwa tayari kumpokea Yesu maishani mwao.

Rafiki yangu, je!  Umekuwa na mabadiliko hayo moyoni?  Je!  Uko tayari kuachana na dhambi inayozinga nafsi yako?  Kwa jina la Yesu, tubu, badilisha mwenendo wako na dhambi zako zitasamehewa.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.