Kushinda Vizuizi
Add to FavouritesWarumi 8:35-37 Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga? Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa. Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.
Nadhani sote tungekubaliana kinadharia kwamba mateso, tukiyapokea vilivyo, yanaweza kutengeneza na kuboresha tabia yetu. Lakini mateso yakimfikia mtu mwenyewe, kumbe nadharia na utendaji yanaachana kabisa!
Maishani, mara nyingi, inatubidi tushinde vizuizi – madoa yaliyochafua nafsi kwenye kiini cha moyo pamoja na uvamizi unaotoka nje.
Sijui kama umeshagundua jinsi mtu anajisikia kuwa peke yake wakati anajitahidi kushinda? Mashaka yanaingia, wengine hawaelewi unayoyapitia halafu unajisikia kwamba huna nguvu pia.
Ungesemaje nikikwambia kwamba hapo hapo uliopo unakuwa na fursa kubwa mno kutoka kwa Mungu?
Warumi 8:35-37 Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga? Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa. Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.
Mtume Paulo alikuwa anateswa vibaya sana, daima uhai wake ulikuwa hatarini wakati aliandika maneno haya. Je! Ungeweza kuandika hivyo katika mazingira yale? Lakini yeye Aligundua mwenyewe kwamba katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.