Kustahimili Katika Dhiki
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.
Warumi 12:12 Kwa tumaini, mkifurahi; katika dhiki, mkisubiri; katika kusali, mkidumu.
Sijui kama umeshaona jinsi muda unavyojivuta polepole unapopitia mateso? Viumbe vingine vinaendelea kwa kasi zao za kawaida, lakini kwa ajili yako, kila sekunde inaonekana kupita taratibu sana. Ndiyo maana subira huisha haraka. Mambo haya ya dhiki hayajaisha? Kwa nini huwezi kuvuka upande wa pili?
Fundi saa wa kutoka Uholanzi, Corrie ten Boom, alikuwa mama aliyeweza kuokoa Wayahudi wengi wasikamatwe na wa-Nazi wakati wa Vita ya Pili ya Dunia. Hatimaye, yeye mwenyewe alikamatwa na kutumwa kwenye kambi ya Ravensbruck. Katika mazingira ya kifo, magonjwa, na ukatili usioelezeka, aliweza kustahimili hali hiyo akiwa na roho ya amani na utulivu.
Yeye na dada yake Betsie, aliyekufa hatimaye pale pale, waliomba pamoja, wakashirikishana masomo ya Biblia na kuhudumia wengine. Baadaye, Corrie aliandika hivi:
“Hakuna shimo ndefu kupita kina cha upendo wa Mungu.”
Hakuweza kuepuka mateso au dhiki; bali alivistahimili akiwa na tumaini na imani kwa Mungu wa milele.
Bila shaka, hatuwezi kufikiria mateso aliyopitia Corrie na uvumilivu wake. Lakini hata sisi, katika hali tunazopitia, tunaweza kuwa na utulivu, amani, na imani kama ile ya Corrie — si kwa sababu mimi nimesema, bali kwa sababu ndivyo Mungu alivyosema:
Warumi 12:12 Kwa tumaini, mkifurahi; katika dhiki, mkisubiri; katika kusali, mkidumu.
Rafiki yangu, kuna nguvu kubwa ndani ya Neno la Mungu. Dua yangu kwa ajili yako leo ni hili: katika muda huu, pale ulipo, uweze kuona nguvu hiyo ndani yako, ukifurahia tumaini thabiti ulilopewa kupitia Yesu Kristo, ili uweze kushikilia subira ya ki-Mungu katika mateso yako. Uone kwamba hakuna shimo ndefu kupita kina cha upendo wa Mungu.
Katika dhiki, uwe na subira.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.
