... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

kuwa wa kwanza

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

MIthali 17:27,28 Azuiaye maneno yake ni mwenye maarifa; na mwenye roho ya utulivu ana busara. Hata mpumbavu akinyamaza, huhesabiwa hekima; akifumba midomo yake, huhesabiwa ufahamu.

Listen to the radio broadcast of

kuwa wa kwanza


Download audio file

Inawezekana wewe au mimi hatutakuwa wenye kukimbia mbio kuliko wengine, wala kuwa aliye na akili zaidi au atakayepata mafanikio kati ya kundi.  Lakini kuna kitu ambacho kitatufanya tuwe wa kwanza.  Je!  Ungependa kujua ni kipi?

Rafiki yangu aitwaye Peter Sewell aliniambia habari yake hii hivi karibuni: “Wakati nilikuwa mtoto wa umri wa miaka mitano, nilikimbia katika mashindano shuleni siku ya sherehe.  Lakini watoto wengine wote walisimama kabla ya kufikia mwisho pale palipokuwa kamba.  Nilikuwa wa mwisho lakini nilifululiza na kukata kamba na kupata ushindi!  Ni kwa sababu nilikuwa mtoto makini wa kusikiliza vizuri na kufuata maelekezo.”

Habari hii inapendeza, si kweli?  Shida ni kwamba wengi wetu hatuko hivvyo.  Laiti ningeweza kurudi nyuma na kurejea katika ujana wangu na kutoa ushauri kwangu mimi mwenyewe.  Ningetoa ushauri huu:  Berni, kaa chini, fumba midomo yako halafu usikilize.

Kuongea sana bila kusikiliza ni kazi isiyo na faida…

MIthali 17:27,28  Azuiaye maneno yake ni mwenye maarifa; na mwenye roho ya utulivu ana busara.  Hata mpumbavu akinyamaza, huhesabiwa hekima; akifumba midomo yake, huhesabiwa ufahamu.

Ni mara ngapi tunaanza kuongea tu, au kukimbia bila kusikiliza kwanza?  Anachotwambia Mungu katika mistari hii ni kwamba, kadiri tunavyopunguza maneno yetu na kutathmini wanayoyasema wengine na kujaribu kuangalia mambo kwa mtazamo wao – ndipo tutakapozidi kuwa na hekima.

Wengi wetu tunataka Mungu abadilishe maisha yetu; lakini ni wachache wanaweza kuchukua muda wa kumsikiliza.  Labda wewe hauko mwepesi kwa kukimbia.  Lakini nisikilize, bado unaweza kuwa wa kwanza katika mashindano.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.