... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Maelekezo ya Kufanya Amani (4)

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Wakolosai 3:15,16 Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani. Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkufundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.

Listen to the radio broadcast of

Maelekezo ya Kufanya Amani (4)


Download audio file

Sawa.  Sasa mtu atawezaje kweli kweli kuwa na utulivu na amani ya Mungu – hali ambayo hata wewe unashauku nayo –Saa Mtu anawezaje kuwa na hali hiyo?

Mimi ni jamaa anayependa mambo halisi.  Ndio maana huduma yetu inaitwa “Christianityworks” yaani Ukristo unafanyakazi.  Unafanya kazi kweli, Na kama haufanyi kazi, inabidi tuuache na kufanya mambo mengine kwa kuwa tutakuwa tunapoteza muda bure.

Kwa hiyo, Mungu anatuahidi kutupa amani katikati ya misukosuko (na hii amefanya mara nyingi ndani ya Biblia), mimi ninaamini kwa moyo wangu wote kwamba inabidi tushikilie amani ile katika maisha ya kila siku.  Ebu sikiliza …

Wakolosai 3:15,16  Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani.  Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkufundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.

Ni kweli, ruhusu amani ya Kristo kutawala mawazo yako – iongoze moyo wako.  Lakini kwa njia gani?  Sikiliza tena: 

Tena iweni watu wa shukrani – kwa sababu rafiki yangu, mtu akiwa na shukrani kwa yote Mungu aliyomtendea, ni msimamo wenye uwezo wakubadilisha kabisa mtazamo wake katika yote. kunamfungulia moyo aweze kupokea na kuhifadhi mafundisho ya Kristo kwa wingi.

Kwa maneno mengine ni kusema, ingiza Neno la Mungu moyoni kila wakati.  Litafakari, licheue, ushibishwe nalo.  Ruhusu wengine wakufundishe na kukuonya katika hekima ya ki-Mungu halafu umwimbie Mungu wimbo mpya kutokana na moyo wa shukrani.

Hii ndiyo njia ya kujua na kupata amani ya Mungu siku baada ya siku.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.