... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Maneno Mapya

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Zaburi 33:4,5 Kwa kuwa neno la BWANA lina adili, na kazi yake yote huitenda kwa uaminifu. Huzipenda haki na hukumu, nchi imejaa fadhili za BWANA.

Listen to the radio broadcast of

Maneno Mapya


Download audio file

Haijalishi unaongea lugha gani nyumbani, maneno mapya na sentensi mpya vinaongezwa kila wakati kwenye kamusi yako kuliko unavyofikiria.  Lakini hilo si jambo jipya.

Baba wa Taifa, Julius Nyerere, wakati wa uhuru, alisisitiza wananchi watumie lugha ya taifa, wasitegemee kuingiza Kiingereza kila mara katika Kiswahili bali maneno mapya yaundwe yanayoendana na maendeleo.  Kwa hiyo leo tuna maneno kama “tarakinishi”, “utandawazi”, “chapishi” na kadhalika.

Kwa kuwa siku hizi dunia inaenda kasi, tutaendelea kupata maneno mapya kupitia mtandao yanayoendana na mfumo wa kidijitali, maneno yanayoeleza fadhaa zinazotawala mioyo ya watu wengi.

Tumeachana na mambo ya zamani.  Tunakumbana na changamoto ambazo mababu kamwe wasingeweza kutabiri.  Ndiyo maana ni rahisi kufikiri kwamba mtazamo wetu unaohusu jamii na mawazo yetu ya kisasa ni bora kuliko vya kale.

Ila, mengi ya mambo tunayoita “maendeleo” yanaharibu maisha ya watu wengi kabisa; yanavunja ndoa; yanafanya watoto wakose baba mzazi; yanatupia mbali maadili kama takataka.  Lakini …

Zaburi 33:4,5  Kwa kuwa neno la BWANA lina adili, na kazi yake yote huitenda kwa uaminifu.  Huzipenda haki na hukumu, nchi imejaa fadhili za BWANA.

Hailishi unaongea lugha gani au unaishi wapi au unafanya kazi gani … usitupe Neno la Mungu.  Lina adili, ni kweli.  Linataja uwaminifu wake, wema wake na haki yake – viweze kuingizwa mioyoni mwetu.  Katika ulimwengu wetu huu unaozidi kuvurugika, si kila wazo jipya linaloweza kuleta maendeleo mazuri.

inatubidi turejee kwenye msingi ili tuweze kugundua kwamba nchi imejaa fadhili za BWANA. 

Na Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.