... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Mungu yu Karibu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Zaburi 145:17-20 BWANA ni mwenye haki katika njia zake zote, na mwenye fadhili juu ya kazi zake zote. BWANA yu karibu na wote wamwitao, wote wamwitao kwa uaminifu. Atawafanyia wamchao matakwa yao, naye atakisikia kilio chao na kuwaokoa. BWANA huwahifadhi wote wampendao, na wote wasio haki atawaangamiza.

Listen to the radio broadcast of

Mungu yu Karibu


Download audio file

Kuna wakati ni vigumu sana kupokea ahadi za Mungu moja kwa moja kama ilivyo.  Mungu ni mwema.  Mungu ni mwaminifu.  Kamwe hawezi kukuacha wala kukupungukia.  Vizuri sana.  Lakini kuna wakati mambo yanaenda kombo, je!  Hayo yote ni kweli?

Inategemeana.  Ni kweli, wema wake Mungu na uwezo wake, upendo wake na uaminifu wake ni hakika kwa kweli.  Lakini inategemeana kama hayo yote tunaweza kuyapokea.  Inategemeana jinsi tunavyomwitikia.

Zaburi 145:17-20  BWANA ni mwenye haki katika njia zake zote, na mwenye fadhili juu ya kazi zake zote.  BWANA yu karibu na wote wamwitao, wote wamwitao kwa uaminifu.  Atawafanyia wamchao matakwa yao, naye atakisikia kilio chao na kuwaokoa.  BWANA huwahifadhi wote wampendao, na wote wasio haki atawaangamiza.

Ukweli usiopingika: BWANA ni mwenye haki katika njia zake zote, na mwenye fadhili juu ya kazi zake zote.  Hakuna majadala.  Lakini je!  Yu karibu na akina nani?  BWANA yu karibu na wote wamwitao, wote wamwitao kwa uaminifu. 

Je!  Naweza kukuuliza jinsi ulivyomwitikia Mungu.  Je!  Umemwita kwa uaminifu?  Unamcha?  Unamlilia?  Unampenda?  Kama jibu lako ni Ndiyo, basi utaweza kupokea ahadi zote alizoahidi.  Utafahamu uwepo wake tele akikukaribia na kukuonyesha upendo wake.

Lakini kama jibu lako ni Hapana, ujue hili:  Wote wasio haki atawaangamiza.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.