Nanga ya Tumaini
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.
Waebrania 6:19,20 Tuliyo nayo kama nanga ya roho, yenye salama, yenye nguvu, yaingiayo hata mle mlimo ndani ya pazia, alimoingia Yesu kwa ajili yetu, mtangulizi wetu, amekuwa kuhani mkuu hata milele kwa mfano wa Melkizedeki.
Tumaini, ukifikiri kidogo, ni hisia lisilo la kawaida kwa sababu kile ambacho tunakitumaini kwa tafsiri ya neno, bado hakina uhakika. Na hatupendi kutokuwa na uhakika, si kweli?
Lakini ingekuaje kama “tumaini” lisingekusudiwa kuwa na tafsiri ya mashaka, hasa tumaini ambalo Mungu analizungum’zia yeye. Katika kazi ninalolifanya, ninakutana na watu wengi mbali mbali. Wengi sana. Asilimia 95% yao wanaonekana kuwa watu wenye uwiano mzuri, wenye furaha kwa ujumla.
Waebrania 6:19,20 Tuliyo nayo kama nanga ya roho, yenye salama, yenye nguvu, yaingiayo hata mle mlimo ndani ya pazia, alimoingia Yesu kwa ajili yetu, mtangulizi wetu, amekuwa kuhani mkuu hata milele kwa mfano wa Melkizedeki.
Mfano huu unaonyesha jinsi Yesu aliingia patakatifu pa patakatifu kupitia pazia nzito iliyokuwa ndani ya hekalu pale Yerusalemu, mahali ambapo Uwepo wa Mungu ulikaa, mahali ambapo Kuhani Mkuu alikuwa na kibali cha kupaingia mara moja tu kila mwaka.
Lakini Yesu amefungua njia ya kumwendea Mungu, nyuma ya pazia kwa ajili ya wewe na mimi, kuanzia sasa hadi milele zote. Ndiyo maana tumaini letu kwake ni hakika, ni imara kama mwamba, kama nanga wakati wa dhoruba.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.