Helping you live the life God intended

Sema Yale Unayomaanisha

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Waefeso 4:14,15 Ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu. Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo.

Listen to the radio broadcast of

Sema Yale Unayomaanisha


Download audio file

Kuna watu huwa wanabadili-badili mawazo yao kulingana na maoni ya mtu wa mwisho waliyezumza naye, au habari ya mwisho waliyosoma.
Ni jambo jema mtu kubadili msimamo wake kwa ushauri mzuri au baada ya kupata maelezo mapya, lakini mtu asiye na msimamo thabiti ana udhaifu mkubwa sana kwa kweli.

Waziri Mkuu wa Uingereza, Neville Chamberlain, alitamani sana amani iendelee kati ya Uingereza na Ujerumani.
Kwa hiyo, aliweza kushawishika kirahisi na ahadi za Adolf Hitler.
Mwaka wa 1938, mjini Munich, Ujerumani, alibadili msimamo wake mara kwa mara kutokana na mazungumzo ya kidiplomasia, hivyo alishindwa kuweka mikakati thabiti.

Upungufu wake wa kukabiliana moja kwa moja na uchokozi wa Wanazi mapema ulimtia moyo Hitler kuanzisha Vita ya Pili ya Dunia mwaka mmoja baadaye.

Labda huo ni mfano mkubwa sana, lakini hata sisi — tukishindwa kuwa na msimamo thabiti na kuueleza kwa uwazi — lazima tujikute kwenye matatizo pia.

Waefeso 4:14-15
Ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.
Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo.

Mungu anataka tuwe watu wa uadilifu, tuzungumze yale tunayomaanisha moyoni, na tusimame kwenye tuliyoyasema.
Maneno yetu yana uzito.
Kusema kweli bila unafiki ni ishara ya maisha ya mtu mwenye kumcha Mungu.

Hata hivyo, hii si kibali cha kuwa wakali au wakatili.
Daima kweli ifunikwe kwa upendo, si iwe kama fimbo ya kuwachapa wengine.
Kupiga chuku, kupinda ukweli au kutumia hila ni udanganyifu.
Mungu anapenda kweli, kwa hiyo anatarajia tuwe watu wa uwazi na wasema kweli.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy