... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Tabia Inayoaibisha

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mariko 9:33,34 Wakafika Kapernaumu; hata alipokuwamo nyumbani, akawauliza, Mlishindania nini njiani? Wakanyamaza; kwa maana njiani walikuwa wakibishana wao kwa wao, ni nani aliye mkubwa.

Listen to the radio broadcast of

Tabia Inayoaibisha


Download audio file

Shauku ya kusifiwa na kupendwa ni siri iliyomo moyoni mwa watu wengi.  Mara nyingi inadhihirika katika maneno yetu na mienendo pia … na ikionekana hivyo, haipendezi.

Je!  Ni vibaya kujitahidi kutenda vizuri iwezekanavyo kushindia jambo fulani?  Si vibaya.  Yaani ni vizuri kufaulu.  Lakini kama tunataka kushinda kwa kumfanya mtu mwingine apate hasara, wakati tunataka kupanda cheo kwa kukandamiza watu wengine, kwa kweli haipendezi hata kidogo.

Je!  Umewahi kuwa na nia hiyo?  Kutaka kumshinda mtu fulani kazini ambaye daima anakupita machoni pa bosi wenu?  Au labda unataka watu wakuone kuwa na akili kuliko mwenzako, kuonekana kwamba wewe unapendeza, au lo lote lile lingine?  Ukiwa na nia kama hiyo, unataka ibaki kuwa siri yako, si kweli?  Na hii ndiyo ilikuwa hali ya wanafunzi wa Yesu wakati habari ifuatayo ikitokea:

Marko 9:33,34  Wakafika Kapernaumu; hata alipokuwamo nyumbani, akawauliza, Mlishindania nini njiani?  Wakanyamaza; kwa maana njiani walikuwa wakibishana wao kwa wao, ni nani aliye mkubwa.

Kwa nini wanafunzi walishindwa kumjibu?  Ni kwa sababu walikuwa na aibu kabisa wakizingatia yale yote waliyoweza kuona na kusikia kwake Yesu hadi wakati huo, wakaelewa kwamba mabishano yao hayafai hata kidogo.

Je!  Utaruhusu nikikuuliza kama wewe una nia ya sirini kutafuta ukubwa kwa kuathiri watu wengine?  Kwa sababu, kama jibu lako ni “ndiyo”, kwa kweli ni aibu.  Na hii ndio sababu unafanya kwa siri. 

Na Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.