... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Utayari wa Kufundishwa

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mithali 1:1-6 Mithali za Sulemani, mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli. Kujua hekima na adabu; kutambua maneno ya ufahamu; kufundishwa matendo ya busara, katika haki na hukumu na adili. Kuwapa wajinga werevu, na kijana maarifa na hadhari; mwenye hekima asikie na kuongezewa elimu, na mwenye ufahamu ayafikie mashauri yenye njia. Kufahamu mithali na kitendawili, na maneno ya wenye hekima na mafumbo yao.

Listen to the radio broadcast of

Utayari wa Kufundishwa

Download audio file

Ebu fikiria, wewe ni mama anayeandaa chakula kitamu, lakini kumbe!  Katikati ya maandalizi yako, unakuta umeishiwa kiambato cha muhimu katika upishi wako.  Unaenda haraka kwenye duka lililo pembeni ya nyumba yako. Lakini wakati unafika pale, kumbe!  Kuna bango mlangoni inayosema, “Samahani, tumefunga”.  Sasa utafanya nini?

Yaani mambo yanataka kukuharibikia!  Unahitaji duka lile liwe wazi, Kwa sababu bila kiambato kile cha muhimu, upishi wako hautawezekana.

Lakini ni mara ngapi sisi tunatundika bango kusema “Tumefunga” wakati inatakiwa tubadilishe mwenendo wetu; wakati inatakiwa kujifunza kitu kipya; wakati ingetubidi tukubali kwamba tumeharibu mambo na ya kwamba matengenezo yanahitajika?

Mimi binafsi, wakati nilikuwa kijana, nilikuwa fundi wa kukwepa ushauri kwa sababu nilijiona kuwa mtu anayejua kila kitu.  Wewe vipi?  Ndiyo maana, zamani Mfalme Sulemani, alifundisha kwa kusema hivi…

Mithali 1:1-6  Mithali za Sulemani, mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli.  Kujua hekima na adabu; kutambua maneno ya ufahamu; kufundishwa matendo ya busara, katika haki na hukumu na adili.  Kuwapa wajinga werevu, na kijana maarifa na hadhari; mwenye hekima asikie na kuongezewa elimu, na mwenye ufahamu ayafikie mashauri yenye njia.  Kufahamu mithali na kitendawili, na maneno ya wenye hekima na mafumbo yao.

Rafiki yangu, kuhusu marudio na mafundisho, uwe umefungua milango yako masaha 24 kila siku ya wiki.  Umsikilize Mungu kwa sababu hekima yake itabadilisha maisha yako.

Na, Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.