... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Uwezo wa Neno Lake

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mariko 1:23-26 Na mara palikuwapo ndani ya sinagogi lao mtu mwenye pepo mchafu; akapaza sauti, akisema, Tuna nini nawe, Yesu wa Nazareti? Je! Umekuja kutuangamiza? Nakutambua u nani, Mtakatifu wa Mungu. Yesu akamkemea, akisema, Fumba kinywa, umtoke. Yule pepo mchafu akamtia kifafa, akalia kwa sauti kuu, akamtoka.

Listen to the radio broadcast of

Uwezo wa Neno Lake


Download audio file

Uovu unatuzunguka kila pande, ukiangalia tu utauona.  Lakini mara nyingi hatutaki kuangalia kwasababu; uovu umezidi mno.  Kwahiyo, tunajikuta tunaendelea na maisha yetu tu.  Lakini kuna sehemu tusingetazamia kuuona,

Uovu ni neno baya linalotisha, kwahiyo; ni mara chache tunaweza kulitumia neno uovu kwa kujitambulisha.  Lakini; mara nyingi sisi wenyewe tunasababisha migogoro; ni upendeleo wetu unaozuia upendo wa Mungu kutembea kwa kupitia sisi kwenda kwa watu wengine; ni ubinafsi wetu unaokuwa kizuizi, si kweli?

Giza iliyomo moyoni inatisha mno.  Na uovu huo (tusikwepe kuuita kama ulivyo!) ndiyo, Yesu alikuja ili atuweke huru, wewe na mimi.  Kuwa huru sasa, ni kutenda mema na kuwapenda wengine bila kuhesabu gharama.  Kuwa huru ili tuwe wale; ambao Mungu alikusudia tuwe na kuleta mabadiliko ulimwenguni kama alivyopanga tufanye.  Lakini je!  Mtu anawezaje kupata uhuru ule?

Mariko 1:23-26  Na mara palikuwapo ndani ya sinagogi lao mtu mwenye pepo mchafu; akapaza sauti, akisema, Tuna nini nawe, Yesu wa Nazareti?  Je!  Umekuja kutuangamiza?  Nakutambua u nani, Mtakatifu wa Mungu.  Yesu akamkemea, akisema, Fumba kinywa, umtoke.  Yule pepo mchafu akamtia kifafa, akalia kwa sauti kuu, akamtoka.

Haijalishi uovu unaonekanaje maishani mwako, Yesu anapotamka kuwa anakuweka huru.  Kama vile alivyosema, “Nikikuweka huru, utakuwa huru kweli kweli.”  Kuna nguvu nyingi sana katika Neno lake.  Uwezo wa kukuweka huru ili uwe yote aliyokusudia uwe.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.