... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Wakati Mtu Anapoteza Vyote

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mathayo 16:24-26 Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona. Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?

Listen to the radio broadcast of

Wakati Mtu Anapoteza Vyote

Download audio file

Nadhani Maisha, ni mvutano kati ya mema na mabaya; kati ya kufanya yale unayojua kuwa sahihi na kufanya yanayokupendeza wewe; kati ya anasa za dunia hii na hazina za mbinguni.

Wewe umechagua nini kati ya kufanya yaliyo sahihi na kufanya yanayokupendeza.  Lakini mtu akichunguza vizuri pande zote mbili na kupiga mahesabu, kwa kweli kuna njia moja tu ya kuendea ambayo inaeleweka vizuri.

Mathayo 16:24-26  Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate.  Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona.  Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake?  Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?

Biashara iliyopo hapa ni uzima wenyewe – uzima wa sasa na wa milele pia.  Kuna faida gani, aliuliza Yesu, kuupata ulimwengu wote lakini huku akipata hasara ya nafsi yako mwenyewe?  Billy Graham aliwahi kujumlisha jibu la mada hii kwa kusema hivi: Wakati mali inapotea, hakuna kilichopotea, wakati afya inapotea, kuna sehemu fulani iliyopotea; wakati maadili yanapotea, kila kitu kimepotea.

Ukiendelea kufikiri kivyako tu, hatimaye utapoteza yote.  Chukua msalaba wako na umfuate Yesu.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.