Yote Yameshikamana
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.
Isaya 64:8 Lakini sasa, Ee BWANA, wewe u baba yetu; sisi tu udongo, nawe u mfinyanzi wetu; sisi sote tu kazi ya mikono yako.
Je! Umewahi kujiangalia kwenye kioo na kujiuliza: “Kama mimi ningejiumba mwenyewe, ningeumba tofauti?” Sisemi sura yako tu, bali hata tabia yako, familia yako, mateso uliyopitia njiani na mazingira yako. Ni mambo gani ungefanya tofauti kama wewe ungekuwa Mungu?
Nadhani sote tunayo mambo ambayo tungetamani Mungu angefanya tofauti wakati alituumba na kutupa uhai wa kuishi maisha yetu hadi leo.
Lakini tujiulize: kwa nini tunataka kumkosoa Mungu, kutilia mashaka maamuzi yake, au kutamani kwamba angeboresha maisha yetu kwa namna fulani?
Sikiliza maneno ya nabii katika Agano la Kale:
Isaya 64:8
Lakini sasa, Ee BWANA, wewe u baba yetu; sisi tu udongo, nawe u mfinyanzi wetu; sisi sote tu kazi ya mikono yako.
Mstari huu, ambao pia ni dua, ni kukiri kwa unyenyekevu kwamba Mungu ndiye anayefinyanga maisha yetu, na kwamba sisi ni mali yake.
Si kwa bahati nasibu ulivyo hivyo ulivyo, wala maisha yako hayajatokea tu bila mpango. Vyote vikuhusuyo vimeundwa na Mungu kwa upendo na kwa makusudi, kama vile mfinyanzi afinyangavyo udongo kutengeneza kitu cha kipekee kwa mikono yake.
Kila kitu kimeunganishwa kwa usahihi—vipaji vyako, mazingira yako, mateso unayopitia, safari yako na hata hatima yako. Mungu bado anakufinyanga.
Kubali kazi yake, kwa sababu wewe ni kazi ya mikono yake.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.
