Changamka kwa Kumtumikia Mungu
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.
Warumi 12:11 Kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana.
Hakuna kinachoweza kusisimua kuliko kuwa na furaha, nguvu, na juhudi katika kutenda kazi inayokufaa, kazi inayotumia vipaji na vipawa vyako vya kipekee kwa manufaa ya watu wengine.
Juhudi ni kama upanga ukatao kuwili. Ikilenga jambo baya, inaweza kuleta madhara makubwa. Lakini ikilenga jambo jema — jambo linalokufaa, linaloendana na vipaji vyako, na kutenda mema katika ulimwengu — jamani, juhudi ile ni kitu kizuri mno!
Pengine hujawahi kufikiria hili: kwa mwaka, ninaandika ujumbe 365 za kipindi hiki cha Neno la Mungu Safi na Lenye Afya, moja kwa kila siku. Kwa wastani, maneno ni 140,000 — sawa na kijitabu kinachoandikwa na daktari chuoni. Huu ni mwaka wa 10 ninaandaa vipindi hivi, na leo ni kipindi namba 3,255. Kila kipindi kinarikodiwa kwenye studio ya redio na pia TV.
Haishangazi nikishoulizwa mara nyingi: Je! Unawezaje kuendelea kuviandaa kila siku, mwaka baada ya mwaka?
Acha nikujibu. Mungu aliniumba nifanye kazi hiyo. Wakati ninaketi asubuhi kuangalia komputa yangu na kuandaa ujumbe unaofuata, moyoni ninafurahia sana. Ninapenda kazi hii — na ndivyo ilivyokusudiwa iwe.
Warumi 12:11
Kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana.
Katika lugha ya asili ya Kigiriki, neno “juhudi” linaleta picha ya maji kuchemka. Uchangamke kama vile maji yanapobubujika na kutoa mvuke mwingi. Rafiki yangu, ukigundua na kutumia vipaji na vipawa ulivyokirimwa na Mungu wakati alikuumba, utachangamka kabisa katika kazi yako yote ile.
Changamka katika kumtumikia Mungu!
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.
