Kumbuka Thawabu Yako
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.
Wakolosai 3:23,24 Lo lote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu, mkijua ya kuwa mtapokea kwa Bwana ujira wa urithi. Mnamtumikia Bwana Kristo.
Kujaribu kuvutia watu wengine bila shaka kunaweza kumletea mtu thawabu ya muda mfupi. Ukimpendeza bosi yako yamkini unaweza kuongezewa msharaha au kupanda cheo au vyote viwili. Lakini kuna kitu kilicho muhimu zaidi, muhimu sana na mkubwa ambacho kinachotupasa kuelewa.
Ni sahihi kabisa katika yote ufanyayo kujitahidi kutumika vema iwezekanavyo. Lakini badala ya kutumia vipaji vyako ulivyopewa na Mungu ili uwavutie watu wengine, vitumie kumtukuza Mungu. Hapo ndipo kuna uhuru. Hapo ndipo kuna kuridhika. Na kufanya hivyo kwa kweli, kunaweza kumletea mtu thawabu fulani wa muda mfupi pia.
Lakini bado kuna taswira kubwa mno katika mada hii kwa sababu …
Wakolosai 3:24 Mkijua ya kuwa mtapokea kwa Bwana ujira wa urithi. Mnamtumikia Bwana Kristo.
Sasa naomba uwe wazi. Kama ungepewa nafasi ya kuchagua kati ya kupata thawabu kutoka mtu fulani uliyemvutia au kupata thawabu kutoka kwa Mungu (ama katika maisha haya ama baadaye katika umilele) ni ipi ungependelea kupata? Ni kweli, sisi sote tunaweza kusitasita katika uchaguzi huo – kivutio cha thawabu ya sasa hivi ya muda mfupi kina nguvu kweli.
Kwa hiyo acha nikuulize, je! Ni thawabu gani iliyo kubwa zaidi? Ni yupi awezaye kukupa thawabu izidiyo kwa muda mrefu zaidi (milele na milele)? Ni watu wanaokaa hapa duniani au ni Mungu mwenyewe?
Mkijua ya kuwa mtapokea kwa Bwana ujira wa urithi. Mnamtumikia Bwana Kristo.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.