... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kwa Nini Watu Wanajichosha Hivi?

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mhubiri 4:4 Tena nikafikiri amali zote, na kila kazi ya ustadi, ya kwamba inatoka katika mtu kupingana na mwenzake. Haya nayo ni ubatili na kujilisha upepo.

Mimi kama mtu anayekubali kwamba lazima tujitahidi kazini (kama ninavyofanya mimi mwenyewe!) nimegundua sasa kadiri ninavyozidi kuzeheka na kuongezeka busara, naona kama kujichosha kazini kunaweza kuleta athari yenye hatari. Nilitaka leo tuongee kuhusu hatari hiyo.

Shauku ya mafanikio ndiyo inayoendesha ulimwengu wa siku hizi, katika maisha ya watu wengi.  Na kwa sehemu, ni sahihi mtu kutafuta ustadi katika kazi anayoifanya. Lakini watu wengi sana (na mimi nilikuwemo zamani) wanaweza kujisahau na kuacha yaliyo muhimu zaidi maishani – yaani ndoa, kujali watoto, kusaidia jamii – kwa sababu wanataka kupata mafanikio kazini tu. 

Sasa inabidi tujiulize mara kwa mara, je! Kwa nini watu wanajichosha kazini?  Au mtu ajiulize mwenyewe, Kwanini mimi ninajichosha hivi?  Na kama umejiuliza maswali kama hayo, jua ya kwamba wewe si mtu wa kwanza kuyauliza.  kweli, miaka elfu tatu iliyopita, Mfalme Sulemani aliandika maneno yafutatayo: 

Mhubiri 4:4  Tena nikafikiri amali zote, na kila kazi ya ustadi, kwa kwamba inatoka katika mtu kupingana na mwenzake.  Haya nayo ni ubatili na kujilisha upepo. 

Kwa hiyo ninataka kukuuliza swali gumu.  Kama wewe ni mtu mwenye mwelekeo wa kujichosha kupita kiasi, je!  Ni kwa sehemu gani?, ukiwa muwazi kabisa, ni kwa sababu ya wivu mtupu,  Ni kwa sehemu gani inatokana na kupingana na wengine wasikuzidi mali, hmm?

Tahadhari:  Haya nayo ni ubatili na kujilisha upepo.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.