... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Hatia ya Kusababisha Ajali

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Kumbukumbu 22:8 Utakapojenga nyumba mpya, fanya ukuta kando-kando ya dari lako, usije ukaleta damu juu ya nyumba yako, mtu akianguka huko.

Katika nchi nyingi, kuhakikisha usalama na afya ya wafanyakazi ni jambo muhimu sana na ni sahihi kuvishugulikia kisheria kwa sababu hua kunatokea ajali za ajabu zinazoathiri wafanyakazi wengi.

Mwaka wa 1993 kulitokea moto kwenye kiwanda cha kutengeneza vidude vya kuchezea watoto huko Thailand kwenye mji wa Bangkok.  Na huu ulikuwa moto mbaya Zaidi kwenye viwanda katika historia.  Moto mdogo ulioanzia chini ulienea haraka kwenye gorofa zote kwa sababu ya makosa kwenye ramani ya jengo lenyewe pamoja na kukosa milango ya dharura ya kutokea kwa haraka.  Watu 188 waliteketea pale pale, wengine 500 walijeruhiwa vibaya.

Hii ni balaa!  Matajiri waliosimamia kiwanda kile, wangewezaje kuzembea hivyo na kusababisha vifo hivyo vitokee?  Kweli wangestahili kufungwa gerezani!

Kanuni ya msingi hapo ni kwamba tunawajibika kuwa waangalifu sana katika kujali watu wengine na kuwalinda.  Yaani, yatupasa kufikiria mapema na kuleta kinga madhara yasiwapate.  Na hata kama imewachukua miaka mingi nchi mbali mbali kupitisha sheria za kulinda wafanyakazi, dhana hiyo ilikuwepo tangu enzi za kale.

Kumbukumbu 22:8  Utakapojenga nyumba mpya, fanya ukuta kando-kando ya dari lako, usije ukaleta damu juu ya nyumba yako, mtu akianguka huko.

Acha nikuulize, je!  Katika maisha yako ya kila siku, unafikiria na kupanga kiasi gani kulinda usalama wa watu wengine?  Labda si swala la kuzuia wasianguke kwenye dari lako, lakini labda kuwalinda hatari zingenezo kama vile kuonewa, kuangukia ndani ya migogoro na mambo mengine ambayo yangewaathiri.

Mtu akiona jambo ambalo lingeweza kumwathiri mtu mwingine lakini akapuuza, atakuwa ana hatia kabisa.  Atakuwa na hatia ya madhara yaliyompata mtu yule.   

Na Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.