... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Acha Tabia ya Kupenda Kucheza na Hatari Hadi Karibu Kabisa

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

2 Timotheo 2:20,21 Basi katika nyumba kubwa havimo vyombo vya dhahabu na fedha tu, bali na vya mti, na vya udongo; vingine vina heshima, vingine havina. Basi ikiwa mtu amejitakasa kwa kujitenga na hao, atakuwa chombo cha kupata heshima, kilichosafishwa, kimfaacho Bwana, kimetengenezwa kwa kila kazi iliyo njema.

Listen to the radio broadcast of

Acha Tabia ya Kupenda Kucheza na Hatari Hadi Karibu Kabisa


Download audio file

Tukiwa watoto, tunawachezea wazazi na kuwajaribu ili tutambue mipaka yao na jinsi tunavyoweza kuwaendesha, tukipima kuona ni wapi tunapoweza kufikia katika fujo yetu.  Ni sehemu ya ukuaji wa mtoto.

Sasa, tukiwa watu wazima, nadhani tumeshaachana na hali hiyo.  Lakini kumbe!  Watu wengi bado wanaendelea kumchezea Mungu, wakijaribu kucheza na hatari hadi karibu kabisa.  Badala ya kuuliza, “Je!  Ninawezaje kumheshimu Mungu kuliko yote?”; wanajiuliza, “Je!  Ninawezaje kuchezea dhambi bila kuadhibiwa?”

Je!  Tunafikiri kwamba Mungu ni mjinga?  Kwamba haoni?  Kwamba hakuna matokeo?  Ukweli ni kwamba Mungu ameandaa mibaraka yake bora kwa ajili ya watu wanaomheshimu.

2 Timotheo 2:20,21  Basi katika nyumba kubwa havimo vyombo vya dhahabu na fedha tu, bali na vya mti, na vya udongo; vingine vina heshima, vingine havina.  Basi ikiwa mtu amejitakasa kwa kujitenga na hao, atakuwa chombo cha kupata heshima, kilichosafishwa, kimfaacho Bwana, kimetengenezwa kwa kila kazi iliyo njema.

Tuanze kufikiria habari ya vyombo vya mti na vya udongo vinavyokuwa kwa ajili ya matumizi “yasiyo ya heshima”.  Pengine ni vyombo vya kuweka taka-taka, hata vingine vya kupeleka choo.  Ni hatari!  Lakini nyumbani pale pale kunaweza kupatikana vyombo vya dhahabu na fedha vilivyotakaswa, vimfaacho Bwana, vilivyotengenezwa kwa kila kazi iliyo njema.

Sasa, wakati wewe bado unatafakari picha hizi mbili, turejee tabia ile ya kupenda kucheza na hatari hadi karibu kabisa hata kwa Mungu, mtu akimjaribu Mungu aone mipaka yake inapofikia wapi.

Swali:  Je!  Katika mifano hii miwili, ungependa kufanana na chombo gani?  Ni wazi, si kweli?  Kwa hiyo acha tabia ile ya kupenda kucheza na hatari hadi karibu kabisa.  Ujitakase na mambo ya aibu kwa sababu kwa vyo vyote, lazima matokeo yawepo. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.