... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Usiuinamie Uovu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Danieli 3:4b,5,6 Enyi watu wa kabila zote, na taifa, na lugha, mmeamriwa hivi, wakati mtakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, lazima kuanguka na kuiabudu sanamu ya dhahabu, mfalme Nebukadreza aliyoisimamisha.

Listen to the radio broadcast of

Usiuinamie Uovu


Download audio file

Siku hizi, ulimwengu unazidi kujaribu kutulazimisha sisi watu wa Mungu, kuinamia uovu; kuacha kuukemea, tuukubali, hata kuupongeza.  Halafu matokeo kwa wasiotii, yanazidi kuwa hatari kabisa.

Hali hiyo nimeishuhudia sana kwetu, na popote unapoishi, bila shaka na wewe umeishuhudia kwenye mazingira yako pia.  Inaonekana kwamba hali ya kuudhiwa na kuteswa kwa Wakristo inaongezeka.  Lakini kwa kweli hii si jambo jipya.

Zamani, wakati Israeli walikuwa wametekwa nyara na kuwa watumwa huko Babeli kwenye karne ya 6 kabla ya Kristo, mfalme wa Babeli, Nebukadreza, alishurutisha watu wainamie na kuabudu sanamu kubwa ya dhahabu iliyofananishwa na sura yake mwenyewe. 

Danieli 3:4b,5,6  Enyi watu wa kabila zote, na taifa, na lugha, mmeamriwa hivi, wakati mtakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, lazima kuanguka na kuiabudu sanamu ya dhahabu, mfalme Nebukadreza aliyoisimamisha. 

Danieli na wenzake walikataa na kama alivyoamuru, Nebukadreza aliwatupa kwenye tanuru ya moto.  Kama tayari unafahamu hatima ya habari hii, utajua kwamba Mungu aliingilia kati na kuwaokoa kimuujiza.  Lakini si kwamba hua inatokea hivi kila mara. 

Baada ya makarne mengi, Yesu naye alikataa kuinamia uovu.  Walimsulubisha!  Hata ikiwaje, hata ikitokeaje, hata ikikugharimu sana, usiuinamie uovu.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.