... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kiburi cha Kishetani

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Luka 4:5-7 Akampandisha juu, akamwonyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja. Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo. Basi, wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako.

Listen to the radio broadcast of

Kiburi cha Kishetani


Download audio file

Je!  Shetani amewahi kukushawishi na kukujaribu moja kwa moja ufikirie kwamba wewe unaweza kuwa mtu maarufu, mtu aliyefanikisha mambo yake vizuri?  Ujue kwamba si wewe tu uliyeweza kujaribiwa hivyo!

Kwa kweli maishani kuna nafasi nyingi ya kutumia fursa ya kupiga hatua.  Hata kama unaona haulingani na wengine kwa sababu ya mapungufu yako, bado nafasi ipo.  Hata kama mambo hayaendi kama ulivyotazamia na umefeli na sasa unajaribu kuyakarabati, bado nafasi ipo.

Fursa hua zinaendelea kupiga hodi kwake mtu.  Kwa kweli, wakati mtu anajisikia vibaya vibaya, kama inavyowatokea watu wote mara kwa mara, fursa zile zina kivutio kikubwa.  Ndiyo maana wengi wanadanganywa na matapeli wanaoahidi kwamba wanaweza kuwaonyesha njama ya kupata mali haraka. 

Yesu alikuwa amekaa siku arobaini jangwani.  Kipindi kile hakula cho chote.  Alikuwa mdhaifu. 

Luka 4:5-7  Akampandisha juu, akamwonyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja.  Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo.  Basi, wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako.

Kuna mwandishi na mnenaji aitwaye Joshua Botella aliyesema hivi, Kama Shetani hawezi kukuangusha, basi atajaribu kukuvimbisha na kiburi.  Usikubali.  Baki mnyenyekevu. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.