... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Zichukie Dhambi Zako

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Timotheo 1:15,16 Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa, ya kwamba Kristo Yesu alikuja ulimwenguni awaokoe wenye dhambi; ambao wa kwanza wao ni mimi. Lakini kwa ajili hii nalipata rehema, ili katika mimi wa kwanza, Yesu Kristo audhihirishe uvumilivu wake wote; niwe kielelezo kwa wale watakaomwamini baadaye, wapate uzima wa milele.

Listen to the radio broadcast of

Zichukie Dhambi Zako

Download audio file

Ni ajabu jinsi tunavyowahukumu watu wengine tukikosoa mienendo yao mibaya wakati hatuoni madhaifu na mapungufu yetu.  Bora tungechukia dhambi zetu kama vile tunavyochukia dhambi za watu wengine.

Si ndivyo tulivyo, jamani?  Wengine wanatusumbua, kwa hiyo tunawahukumu na kuanza kubini jinsi tutakavyowalipiza kisasi.  Hata kama hatulipizi kisasi, bado tunawanung’unikia moyoni.  Bado tuna kinyongo moyoni tukifikiri kwamba mtazamo huo ni sawa machoni pa Mungu.

Ndiyo maana unyenyekevu wake Mtume Paulo unavutia sana:

1 Timotheo 1:15,16  Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa, ya kwamba Kristo Yesu alikuja ulimwenguni awaokoe wenye dhambi; ambao wa kwanza wao ni mimi.  Lakini kwa ajili hii nalipata rehema, ili katika mimi wa kwanza, Yesu Kristo audhihirishe uvumilivu wake wote; niwe kielelezo kwa wale watakaomwamini baadaye, wapate uzima wa milele.

Kabla hajakutana na Yesu, Paulo alikuwa mkorofi kabisa.  Aliwatesa Wakristo bila huruma.  Lakini baada ya kuonana na Yesu ana kwa ana, aligundua kwamba yeye ndiye mwenye dhambi wa kwanza kuliko wenye dhambi wote, lakini hata hivi Yesu alikuja kumwokoa.

Kwa kweli, mara nyingi, dhambi yetu ni mbaya sana kuliko dhambi za wale ambao tunaowahukumu kwa ukali.  Hata hivi, au tuseme, kwa ajili ya hali hiyo, Yesu alikuja akuonyeshe rehema zake pale Msalabani;  yaani uvumilivu usio na mpaka, akichukuliana na madhaifu yako.

Acha kuhukumu wengine. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.