... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Thibitisha Mafanikio Yako

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yoshua 1:8 Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani wako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakaposistawi sana.

Listen to the radio broadcast of

Thibitisha Mafanikio Yako


Download audio file

Leo tunataka kuongea kuhusu mada ya mafanikio.  Mafanikio yako katika ufalme wa Mungu.  Kama una mashaka, ni vizuri, kwa sababu ukimsikia mtu akichanganya Neno la Mungu na “mafanikio”, lazima ujihadhari.

Wakati unasikia neno “mafanikio”, je!  Unawaza nini kichwani mwako?  Kuwa na pesa nyingi?  Nyumba ya fahari?  Gari iliyo bora?  Kuwa na uwezo wa kutalii?  Kupandishwa cheo kazini?  Heshima?  Kujulikana?  Je!  “Mafanikio” yana maana gani kwako?

Si kwamba mambo hayo ni mabaya, lakini kama tunafikiri kwamba ndiyo maana ya mafanikio katika Ufalme wa Mungu, tutakuwa tumejiingiza katika mtego.  Ni hatari kabisa kama tunadhani kwamba Mungu anataka kutukirimia na vipambo hivi vidogo vya thamani ndogo.

Ni kweli, Mungu hua anawabariki watu wake kwa njia hiyo, lakini siyo lengo lake hasa.  Hayo yote hayamo kabisa katika mawazo yake wakati yeye anafikiri habari ya mafanikio.

Wakati Yoshua aliposhika nafasi ya kuongoza Israeli badala ya Musa, na kuwaingiza ndani ya nchi ya ahadi kwa mapigano mengi, Mungu alimwambia maneno yafuatayo:

Yoshua 1:8  Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani wako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakaposistawi sana.

Mafanikio anayaongea Mungu hapa ni kukamilisha mipango na malengo yake, si mipango yake Yoshua.  Kama vile Yesu alisema baada ya makarne mengi, “Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe, mapenzi yako yatimizwe …”

Ni kipi kinachothibitisha mafanikio hayo?  Ni kupokea Neno la Mungu ndani ya moyo, kulitafakari na hatimaye kuwa na mwitikio wa kulitii.  Hapo ndipo mtu anaweza kupata hekima.  Hapo ndipo mtu anaweza kupata mafanikio katika kuyatimiza yale yote Mungu amemwagiza ayafanye.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.