... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kuna Nguvu Katika Ahadi Ile

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Matendo 1:8 Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.

Listen to the radio broadcast of

Kuna Nguvu Katika Ahadi Ile


Download audio file

Je!  Ni lengo gani Mungu aliyeweka mbele yako tangia leo hadi siku utakapovuta pumzi kwa mara ya mwisho?  Kwa nini amekuacha uendelee kuwepo hapa duniani badala ya kukupeleka nyumbani kwake katika utukufu?

Ni maswali yenye changamoto kwa sababu wakati sisi tunamezwa na pirika za kila siku na shughuli zinazohitajika kupambana na maisha haya, ni rahisi kwetu kuacha kulenga mipango ya Mungu na kuelekeza mawazo yetu yote kwenye mahitaji yetu, na tukisema ukweli, matamanio yetu ya kupata starehe na anasa.

Lakini kama wewe ni mmoja wa wale ambao watu wa dunia wanafikiri kwamba wamechanganyikiwa, yaani watu kama mimi ambao wamejitolea mahanga kumfuata Yesu na kumwabudu … hatuwezi kamwe kuhamisha mawazo yetu yalenge mambo yetu tu, haiwezekani.

Baada ya Yesu kufa na kufufuka tena na kupaa mbinguni, wale wanafunzi wangeweza kujiuliza hivi, Basi, hayo yote tuliyoyashuhudia yalikuwa ya ajabu kabisa!  Sasa, kwa nini tusirejee nyumbani, tukalale kila mmoja kwa kitanda chake na kuendelea na maisha yake na kuishi katika starehe hadi uzee wake akiwa na kumbukumba nzuri ya Yesu?

Lakini hakuna uchaguzi kama huo Yesu aliyewapa!  Bali aliwaambia hivi

Matendo 1:8  Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.

Yesu aliwaacha wanafunzi wake hapa duniani ili waende kutangazia ulimwengu habari za upendo wake.  Pia, aliwaahidia uwezo, uwezo wa kweli, uwezo wa Roho Mtakatifu, wawezeshwe kutimiza malengo hayo hayo.

Rafiki yangu, Yesu hakukuacha hapa duniani ili uwe na maisha shwari hadi kustaafu, bali anataka utangaze upendo wake ulimwenguni.  Halafu amekuahidi kwamba Roho Mtakatifu atakupa uwezo wa kutimiza lengo hilo. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.