... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Mpango Kwa Ajili ya Kesho

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Luka 12:16-19 Akawaambia mithali, akisema, Shamba la mtu mmoja tafiri lilikuwa limezaa sana; akaanza kuwaza moyoni mwake, akisema, Nifanyeje? Maana sina pa kuyaweka akiba mavuno yangu. Akasema, Nitafanya hivi; nitazivunja ghala zangu, nijenge nyingine kubwa zaidi, na humo nitaweka nafaka yangu yote na vitu vyangu. Kisha, nitajiambai, Ee nafsi yangu, una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi; pumzika basi, ule unywe, ufurahi.

Listen to the radio broadcast of

Mpango Kwa Ajili ya Kesho


Download audio file

Si ajabu hii, kwamba hata kama tunajua ya kuwa siku moja tutaondoka kutoka maisha haya na kuingia maisha mengine, kila siku tunafikiri na kutenda kana kwamba tutaishi hapa duniani milele.  Tunayo mipango kwa ajili ya kesho, juma lijalo, mwezi ujao, hata mwaka ujao.  Lakini hata hivi siku moja, ratiba zile zote tulizozipanga na kuziandika kwenye kalenda yetu zitakuwa hazina maana tena.

Kwa hiyo, swali ambalo linatakiwa tujiulize ni hili: Je!  Niko tayari kuondoka?  Nijibu, je!  Umejiandaa?  Kwa sababu hata kama sisi sote tunatamani kuishi maisha mazuri marefu, labda hii si mpango wa Mungu hata kidogo.

Je!  Unakumbuka mithali ya Yesu kuhusu tajiri mpumbavu ambaye shamba lake lilikuwa limezaa sana?

Luka 12:16-19  Akawaambia mithali, akisema, Shamba la mtu mmoja tajiri lilikuwa limezaa sana; akaanza kuwaza moyoni mwake, akisema, Nifanyeje?  Maana sina pa kuyaweka akiba mavuno yangu.  Akasema, Nitafanya hivi; nitazivunja ghala zangu, nijenge nyingine kubwa zaidi, na humo nitaweka nafaka yangu yote na vitu vyangu.  Kisha, nitajiambia, Ee nafsi yangu, una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi; pumzika basi, ule unywe, ufurahi.

Tazama anavyoongea jamaa huyu – nitafanya, nitafanya, nitafanya … yaani yote ni mimi, mimi, mimi.  Angalieni jinsi nimepata mafanikio makubwa!  Nitafanya kama nilivyofundishwa na wa ulimwengu huu, nitaweka akiba mali yangu, nitaishi vizuri na nitajifurahisha.

Ni kama alikuwa na mpango kwa ajili ya kila hatua ya maisha yake, kasoro mpango wa umilele.  Kesho tutaangalia ilivyomwendea lakini kwa muda huu, acha nikuulize:  Je!  Uko tayari kuondoka?  Je!  Uko tayari kukutana na Muumba wako? 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.