... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Bila Faida Yoyote

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Luke 9:25,26 Kwa kuwa yamfaa nini mtu kuupata ulimwengu wote, kama akijiangamiza, au kujipoteza mwenyewe? Sababu kila atakayenionea haya mimi na maneno yangu, Mwana wa Adamu atamwonea haya mtu huyo, atakapokuja katika utukufu wake na wa Baba na wa malaika watakatifu

Listen to the radio broadcast of

Bila Faida Yoyote


Download audio file

Mvuto wa vitu vyote ambavyo vinanunuliwa kwa pesa ni kama unaongezeka kila siku.  Yaani mfumo wetu wa uchumi umezidi kuwa stadi kwa jinsi unavyotutenganisha na pesa zetu tulizozitafuta kwa shida.

Simu janja, gari zinazokuwa na viti vyenye kuwekwa baridi au moto, viatu vya fahari, safari za likizo za hali ya juu kabisa … litajwe tu na mtu angeweza kulinunua kwa pesa.

Mama yangu aliishi maisha ya kawaida kabisa.  Hakuwa na vitu vingi, lakini wakati alifariki dunia, mimi ndimi niliwajibika kukusanya vitu vyake.  Tulichunga hiki na kile, lakini nikisema ukweli, karibia vingine vyote tulipeleka dampo.  Hii inasababisha mtu kutafakari sana kuhusu mali aliyo nayo, na jinsi ameambatanisha moyo wake kwayo, na jinsi bado anaweza kutamani apate zaidi, na jinsi hayo yote yanatawala maisha yake.

Luke 9:25,26  Kwa kuwa yamfaa nini mtu kuupata ulimwengu wote, kama akijiangamiza, au kujipoteza mwenyewe?  Sababu kila atakayenionea haya mimi na maneno yangu, Mwana wa Adamu atamwonea haya mtu huyo, atakapokuja katika utukufu wake na wa Baba na wa malaika watakatifu.

Ni kweli kwamba kwa sehemu, kila mmoja wetu anahitaji vitu, ila mtu anaweza kumezwa navyo na kusukumwa na tamaa ya kupata zaidi hadi pale Yesu hapati tena nafasi ya kwanza maishani mwake.  Halafu kadiri mtu anatawaliwa na mali yake na yale bado anayatamani, ndipo nia yake ya kumwishia Yesu, hua inazidi kufifia.  Mpaka anaweza hata kumwonea haya, asitaki tena kuonekana tofauti na waulimwengu kwa ajili yake.

Laiti hali hii isikutokee.  Mali yote uliyo nayo hayatakuwa na faida yoyote siku ile utakaposimama mbele zake katika utukufu wake.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.