... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Hauna Budi Kujaribiwa

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Luka 17:1 Akawaambia wanafunzi wake, Makwazo hayana budi kuja, lakini ole wake mtu yule ambaye yaja kwa sababu yake!

Listen to the radio broadcast of

Hauna Budi Kujaribiwa


Download audio file

Hatupendi kuongea habari ya majaribu kwa sababu, moyoni mwake, kila mtu anadhani ni yeye tu peke yake anayejaribiwa.  Je!  Kwa nini ninayo mawazo haya mabaya?  Je!  Kwa nini tamaa hizi hua zinaendelea kunisumbua?

Acha nitoe mfano:  Umeshindwa na jaribu kubwa halafu wakati unaingia kanisani unaangalia watu wengine na kujisikia kuwa na hatia sana kwa sababu wengine wote wanaonekana kwamba wao ni wakamilifu.  Yaani wanaonekana kwamba hawana tatizo! 

Hapo ndipo Shetani anachochea moto ndani yako kwa kutumia uongo kwamba ni wewe tu.  Huna nguvu.  Hufai kabisa.  Ndiyo maana unajaribiwa!  Wewe ni mnafiki, wewe si Mkristo hata kidogo.  Huna nafasi kuwa katikati ya watakatifu hawa! 

Lazima tupambane moja kwa moja na uongo huo tuufute kabisa.  Kwa kweli, tumruhusu Yesu awe mwenye kukabiliana na uongo huo, kwa sababu … 

Luka 17:1  Akawaambia wanafunzi wake, Makwazo hayana budi kuja, lakini ole wake mtu yule ambaye yaja kwa sababu yake! 

Kesho tutachunguza sehemu ya pili ya mstari huu.  Lakini kwa sasa, tukaze macho kwenye sehemu ya kwanza.  Je!  Yesu alisemaje?  Je!  Ulimsikia vizuri?  Makwazo hayana budi kuja. 

Kumbe!  Kwangu inasikika kuwa dhamana inayotoka midomoni mwa Yesu.  Ukweli ni kwamba, kadiri mtu anakusudia kuishi kwa ajili ya Yesu, ndipo Shetani atazidi kumjaribu. 

Kujaribiwa si dhambi.  Kila mtu ambaye unamfahamu kuwa anampenda Yesu, anajaribiwa sawa sawa na wewe.  Sikia!  Yesu alijaribiwa kama unavyojaribiwa.  Kwa hiyo usimruhusu Shetani akudanganye na uongo wake.  Kwa sababu ukweli ni kwamba makwazo na majaribu hayana budi kuja, lazima yatokee! 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.