... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Nuru Inayoangaza Moyoni Mwako

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Zaburi 119:30 Kufafanusha maneno yako kwatia nuru, na kumfahamisha mjinga.

Listen to the radio broadcast of

Nuru Inayoangaza Moyoni Mwako


Download audio file

Unajua wakati kitu fulani kimekuchanganya muda mrefu sana, yaani unajua kitu hakiko sawa lakini bado hujakielewa ni nini, halafu ghafla, kinaeleweka kwako … ni kama taa imewashwa katika fikra zako.

Siku hizi kuna mhubiri kijana aliyeniomba niweze kumsaidia kutathmini mahubiri yake.  Kwa kweli ilikuwa fursa kubwa kwangu.  Kwa hiyo tuliangalia kwa pamoja video ya hotuba yake ya hivi karibuni, tukiisimamisha na kuianzisha tena, tukiongea hiki na kile, nikimwuliza maswali naye akijitahidi tutafuta majibu.

Naona tulifaulu katika tathmini wakati alisema, “Kumbe!  Ni kama nilihubiri hotuba mbili kwa wakati mmoja!  Ni kama nilijaribu kuambatanisha jumbe mbili tofauti kuwa moja.”  Sawa!  Jambo hilo hilo ndilo nilikuwa ninataka alione.  Ni kama nuru iliwashwa katika akili zake.

Lakini asingelielewa kama asingethubutu kuomba asaidiwe, kama moyo wake usingefunguka kukoselewa kwa nia njema (na unajua kwamba si jambo rahisi).  Na ndivyo ilivyo kwa Neno la Mungu pia.

Zaburi 119:130  Kufafanusha maneno yako kwatia nuru, na kumfahamisha mjinga.

Inatubidi, wewe na mimi, tuwe na moyo wa kujituma kwa kulisoma, kulicheua, kulielewa halafu tukifanya hivyo … ndipo litatia nuru maishani mwetu.

Je!  Ungependelea kuwa mwenye hekima au mjinga?  Je!  Unataka kujifunza, kukua na kubadilika uwe mtu yule Mungu aliyekusudia uwe wakati alikuumba?  Basi, fungua Neno la Mungu, ulisome, ulipokee, ulitafakari na uliitikie.  Litatia nuru maishani mwako.  Litakufanya uwe mwenye hekima.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.