... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Waliotangulia

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

2 Timotheo 1:5,6 Nikiikumbuka imani uliyo nayo isiyo na unafiki, ambayo ilikaa kwanza katika bibi yako Loisi, na katika mama yako Eunike, nami nasadiki wewe nawe unayo. Kwa sababu hiyo nakukumbusha, uichochee karama ya Mungu, iliyo ndani yako kwa kuwekewa mikono yangu.

Listen to the radio broadcast of

Waliotangulia


Download audio file

Katika ulimwengu huu unaosukumwa kasi na teknolojia, ambapo mtu anaweza kuagiza chakula cha jioni kwa kutumia simu yake janja halafu kilaletwa kwake nyumbani baada ya nusu saa, watu hawana muda wa kutafakari siku zao za kale.  Hawakumbuki mema yote yaliyowafanya kuwa kama walivyo leo.

Siku ya leo, katika utamaduni wa China, ni “Siku ya Kufagia Makaburi.”  Labda sisi wengine inasikika tofauti.  Lakini kule, ni desturi kwamba watu wanaadhimisha wazazi walioondoka na mababu kwa kwenda malaloni wakiwa na ndugu zao ili wafagie makaburi yao.  Ni desturi inayokumbusha walio hai kutokusahau kitovu cha maisha yao mazuri na baraka zake.

Najiuliza, je!  Ni mara ngapi unatafakari habari za waliotangulia, waliosawazisha njia kwa ajili yako, waliochangia kukufanya kama ulivyo leo?  Ni kweli, si kila kitu walioweza kuchangia kilikuwa chema, lakini bila shaka vingi vilikufaa kabisa.  Hayo ndiyo Mtume Paulo aliyoweza kumwandikia mfuasi wake katika huduma, Timotheo …

2 Timotheo 1:5,6  Nikiikumbuka imani uliyo nayo isiyo na unafiki, ambayo ilikaa kwanza katika bibi yako Loisi, na katika mama yako Eunike, nami nasadiki wewe nawe unayo.  Kwa sababu hiyo nakukumbusha, uichochee karama ya Mungu, iliyo ndani yako kwa kuwekewa mikono yangu.

Bibi yake Timotheo, aitwaye Loisi pamoja na mama yake Eunike walikuwa na mtikiso mkubwa juu ya imani ya kijana yule.  Usisahau waliotangulia.  Kumbuka walivyojitolea ili uwe kama ulivyo leo.  Uwaheshimu moyoni mwako. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.