... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Bwana Awezaye Kufanya Mambo ya Ajabu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Waefeso 3:20 Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu.

Listen to the radio broadcast of

Bwana Awezaye Kufanya Mambo ya Ajabu


Download audio file

Wakati mtu anafirisika kabisa, hali ambayo inayoweza kumpata kila mtu maishani mwake, kinachoumiza zaidi ni kwamba atakuwa amekatishwa tamaa kupita kiasi.

Wakati mtu anakufa moyo na kukata tamaa ndipo atakuwa amefika kiwango cha chini kabisa.  Wakati mtu hana tumaini tena ujue kwamba amefikia kiwango kile cha chini.  Haoni hata jinsi atakavyoweza kustahimili leo tu, kesho, wiki kesho, mwezi ujao, mwaka ujao. 

Nafahamu vizuri, nimeshapitia kipindi kama hicho.  Labda wewe pia umekipitia.  Hali hiyo inasababisha wengi kujinyonga … Hawaoni sababu ya kuendelea kuishi. 

Kwa ye yote aliyefikia sehemu hiyo mbaya muda huu, au kwa ye yote atakayejikuta siku moja kwamba amekatishwa tamaa hivyo, Mungu anataka kumwambia hivi: 

Waefeso 3:20  Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu. 

Upendo wa Mungu kwako kupitia Yesu Kristo hauwezi kuelezwa kwa maneno ya kibinadamu.  Lakini upo kweli kweli.  Unakuwepo sasa hivi kwa ajili yako.  Pokea upendo wake moyoni mwako muda huu huu kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. 

Rafiki yangu, bado kuna tumaini, kesho utafika.  Kuna hatima nzuri huko mbeleni.  Kwa kweli, nguvu ya upendo wa Mungu ikifanya kazi ndani yako, jua kwamba anaweza kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote uyaombayo au uyawazayo.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.