... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Usimpe Ibilisi Nafasi

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Waefeso 4:26,27 Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka; wala msimpe Ibilisi nafasi.

Listen to the radio broadcast of

Usimpe Ibilisi Nafasi


Download audio file

Sijui kama umeshagundua hili, lakini duniani kuna mambo mengi sana ambayo yangetukasirisha kila wakati.  Wakorofi, mambo ya siasa, mazingira magumu, mitazamo ya watu, yapo mengi tu.

Hasira inapanda wakati mambo yamembana mtu.  Mtu akimwangalia vibaya tu, mara moja anamfokea kabisa.  Ni kweli, kuna mara inatakiwa tukasirike.  Wakati mtu anakusingizia, si una haki kukasirika?  Eeh, ndiyo!

Tusisahau pia kwamba hata kama Mungu si mwepesi wa hasira, hatimaye anaghadhibika.  Lakini kuna mambo mawili kamwe haitakiwi tuyafanye wakati tunakasirika.

Waefeso 4:26,27  Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka; wala msimpe Ibilisi nafasi.

Tusipothibiti hasira yetu, itatutawala, na kitu cha kwanza itakaotupelekea kufanya ni kutenda dhambi; mfano, kufokea watu, kujilipiza kisasi, tukipamba moto kwa kujaribu kutenda kama vile tulitendewa.

Pili, jazba ile itaendelea kutusumbua mchana kutwa, na kwa wengine, hata kusababisha kutokusamehe kwao kuwe kama mzizi wa uchungu … kwa maisha yao yote!  Hii haieleweki.  Kumbe yule uliyokataa kumsamehe anakuwa sasa mtu wa kukushawishi kuliko wote wengine jamani, si kweli?!

Na hali hii inamfungulia Ibilisi mlango kupora maisha yako na kukuangusha kabisa.  Tahadhari:  Usimpe Ibilisi nafasi kupitia hasira yako.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.