... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Uwe Tofauti na Umati wa Watu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mathayo 5:40-42 Na mtu atakaye kukushitaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia. Na mtu atakayekulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye mbili. Akuombaye, mpe; naye atakaye kukopa kwako, usimpe kisogo.

Listen to the radio broadcast of

Uwe Tofauti na Umati wa Watu


Download audio file

Ni huzuni kuikiri, lakini nikikagua moyo wangu, naona kwamba mara nyingi sana, nimekuwa na hisia za kudai haki zangu kila mara.  Ni tabia niliyoirithi kwa kuwa nimezamishwa katika utamaduni wetu hapa ninamoishi.  Sijui wewe ukoje?

Labda ni jambo jepesi kama vile mbwa mdogo anavyobweka jirani.  yule mbwa anapendeza kweli, lakini sauti yake inakuwa kero akiendelea kubweka masaa mengi.

“Nina haki kutulia nyumbani mwangu,” nasema.  Na kweli ninayo haki hiyo nchini kwetu.  Sasa, je!  Nimpelekee malalamiko jirani yangu, au nivumilie tu hadi mbwa atakaokuwa na kuachana na tabia ya utoto?

Jambo la msingi:  Naweza kuvunja uhusiano na jirani au naweza kuuimarisha; naweza kumheshimu Mungu au nimvunjie heshima.  Inategemeana jinsi ninavyoitikia tukio lenyewe.  Yesu alieleza hivi:

Mathayo 5:40-42  Na mtu atakaye kukushitaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia.  Na mtu atakayekulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye mbili.  Akuombaye, mpe; naye atakaye kukopa kwako, usimpe kisogo.

Wakati mtu anakulegezea mambo, wakati anachukuliana nawe, wakati anakuvumilia … je!  Unajisikiaje?  Unamwonaje mtu yule?

Kama kweli unataka kujulikana kwa nia njema, basi msikilize Yesu.  Kubali kwenda ile maili nyingine ya ziada.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.