... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Wakati Unapata Shida

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Zaburi 138:7,8 Nijapokwenda kati ya shida utanihuisha, utanyosha mkono juu ya hasira ya adui zangu, na mkono wako wa kuume utaniokoa. BWANA atanitimilizia mambo yangu; Ee BWANA, fadhili zako ni za milele; usiziache kazi za mikono yako.

Listen to the radio broadcast of

Wakati Unapata Shida


Download audio file

Maishani, kuna wakati ni muhimu sana kusimama kidete juu ya ahadi zake Mungu.  Daima ni muhimu kufanya hivyo lakini hususani wakati wa shida.

Je!  Ni lini uliwahi kukumbana na matatizo, ukakabiliana nayo moja kwa moja?  Adha, mapingamizi, mateso, maumivu, dhiki … haijalishi unayaitaje, shida hua inatikisa imani yako kabisa, inayumbisha imani yako kwa Mungu.  Na mwitikio kama huo ni kawaida kwa mwanadamu.

Ndiyo maana wakati wa shida, ni muhimu mtu asimame kidete juu ya ahadi za Mungu kuliko vipindi vingine.  Tunataka sasa kusoma jinsi Daudi, mfalme wa Israeli, alivyoweka tumaini lake kwake Mungu baada ya kunusurika na matatizo makubwa kuliko wengine:

Zaburi 138:7,8  Nijapokwenda kati ya shida utanihuisha, utanyosha mkono juu ya hasira ya adui zangu, na mkono wako wa kuume utaniokoa.  BWANA atanitimilizia mambo yangu; Ee BWANA, fadhili zako ni za milele; usiziache kazi za mikono yako.

Je!  Utaniruhusu nikikuuliza swali?  Daudi yuko wapi leo?  Hayupo hapa tena.  Hatimaye alifariki dunia kama wengine wote.  Tayari Mungu amepanga muda na kusudi kwa ajili ya kifo chako na kifo changu pia.

Lakini ukichunguza maisha ya Daudi, mara nyingi, Mungu alimpa hekima, na maongozi na moyo mkuu na uwezo wa kuokoka kipindi cha matatizo.

Kwa hiyo, tangu sasa hadi wakati ule atakayekuita kwake, kwa muda mwafaka, Mungu atanyosha mkono wake ili akuokoe na shida.  Fadhili zake kwako, ni za milele.  Hawezi kuiacha kazi ya mikono yake. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.