... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Ulimwengu Bila Upendo

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Wakorintho 13:1-3 Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao. Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi. Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.

Listen to the radio broadcast of

Ulimwengu Bila Upendo

Download audio file

Tujaribu kufikiria ulimwengu bila upendo.  Inatisha, si kweli?  Lakini kwa watu wengi, hawana haja kufikiria sana kwa sababu tayari maisha yao yamekosa upendo kabisa.

Leo hii, kuna watu wengi sana duniani ambao hitaji lao la msingi la kupendwa halipatikani.  Kwa nini?  Ni kwa sababu wamezungukwa na watu ambao hawawapendi.  Wamezungukwa na watu ambao wako bize sana na shughuli zao wenyewe, hawana tena muda kujali wengine kwa sababu wanalenga mipango yao tu, ikiwa mema au mabaya.  Hawana muda wakujishughulisha na shida za watu wengine.

Mimi ninajua kabisa kwa sababu nilikuwa mmoja wa wale watu wanaokosa upendo.  Nilikuwa ninajali mambo yangu tu, sikuwa na muda wa kuonyesha upendo kwa watu walikuwa wananizunguka.  Ilikuwa hasara kwao na iliniletea uharibifu kabisa.  Machoni pa Mungu, hata kama mipango yako ni mizuri namna gani, hata kama umeifanikisha kiasi gani, yote ni bure tu kama huna upendo.

1 Wakorintho 13:1-3  Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.  Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi.  Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.

Sasa katika ulimwengu ambamwo wengi wanakosa upendo, jaribu kuchukua muda wa kuwapenda. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.