... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Inua Macho Yako Uone

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Wafilipi 3:20 Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo.

Listen to the radio broadcast of

Inua Macho Yako Uone


Download audio file

Sasa, niambie; ni mambo gani unayopenda kufanya.  Jambo la kutenga muda kwa kujiburudisha, mambo yanayokupendeza sana?  Mtu anaweza kufurahi hata akiwaza juu ya mambo kama hayo.  Lakini je!  Ni kwa kiasi gani yamekuwa sasa mambo ya kuzubaisha?

Samahani!  Labda nimepunguza furaha yako kwa kusema hivi.  Ulikuwa unafurahia mawazo ya mambo yanayokupendeza sana halafu ghafla … nimeyaharibu kwa kukuuliza swali linalosumbua, swali linalohusu jinsi mambo mazuri yanavyoweza kukuvuta kutoka kwenye kilicho bora, kilicho muhimu kuliko vyote, kile kitu ambacho kitadhihirika kuwa cha msingi mwisho wa maisha yako hapa duniani. 

Labda unafikiri hivi, “Subiri kwanza, si tuliongea swala hili kwenye kipindi cha jana?”  Ndiyo.  Lakini ninataka kukazia hapo.  Ukweli ni kwamba yasiyoonekana ni makubwa na ya muhimu mno kuliko yanayoonekana kwa sababu,  

Wafilipi 3:20  Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo. 

Rafiki, kama unamwamini Yesu, basi wewe ni mpitaji tu hapa duniani.  Nyumbani kabisa ni kukaa naye.  Kwetu, wewe na mimi, ni huko na tuna kila sababu kutazamia kwa shauku kubwa siku ile Yesu atakapokuja au siku sisi tutakapoenda nyumbani kukaa naye. 

Ni rahisi sana kuzubaishwa na mambo ya ulimwenguni, anasa zake pamoja na shughuli zake zote, kiasi mtu anaweza kukosa kilicho muhimu zaidi, yaani kuinua macho yake juu na kuangalia! 

Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo.   

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.