... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Neema ya Ajabu Mno

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yohana 1:16 Kwa kuwa katika utimilifu wake sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema.

Listen to the radio broadcast of

Neema ya Ajabu Mno


Download audio file

Neema inapatikana kwa nadra sana siku hizi.  Mfumo wa ulimwengu huu unatazamia kwamba kila mtu atafanana na wengine, kwamba atakuwa na mchango wake katika jamii.  Yaani inatakiwa wewe utimize sehemu yako, hata ikiwa ndogo, katika kuendesha ile mashini tunaoiita “umma”.

Kama inasikika kuwa utawala wa ki-mabavu, basi chunguza mazingira yako.  Je!  Ni mara ngapi mifumo ya jamii mbali mbali, yaani hekima ya kisasa, ni mara ngapi inaweza kumlegezea mtu?  Ni mara ngapi watu wanaweza kuchukuliana na mapungufu ya watu wengine, sembuse kuwapa fidia na kuwatia moyo?

Ulimwengu tunamoishi imekosa msamaha.  Lazima uwe kama wengine, timiza wajibu wako au toka njiani upishe wengine.  Ni kweli, neema inapatikana kwa nadra sana … isipokuwa, mtu akimgeukia Yesu.

Yohana 1:16  Kwa kuwa katika utimilifu wake sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema.

Ni maneno mazito lakini mazuri sana.  Licha ya makosa yetu, licha ya uasi wetu, au tuseme kwa sababu ya makosa hayo, Mungu alimtuma Yesu ili aweze kutukirimia neema yake, yaani majaliwa yake tusiyoyastahili, mara tena na tena.

Kama vile Billy Graham aliwahi kusema, Mungu, hua anachukua wadhaifu na kuwafanya kuwa wenye nguvu.  Anachukua wachafu na kuwaosha wawe safi.  Anawachukua wenye hali duni na kuwanufaisha.  Anawachukua wenye dhambi na kuwatakasa kabisa .

Ni rahisi kutumia neno “neema” bila kufikiria mara nyingi hadi mtu anaweza kusahau ukubwa wake, jinsi neema inavyopendeza na kuleta matokeo ya milele hapo ikitukirimia mibaraka tele maishani mwetu. 

Acha nikutie moyo leo, umtazame Yesu, uishi mbele zake, ili uweze kuzidishiwa ukipokea neema juu ya neema, juu ya neema.              

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.