... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Alikubali Hayo Yote Kwa Ajili Yako

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Petro 3:18 Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa.

Listen to the radio broadcast of

Alikubali Hayo Yote Kwa Ajili Yako


Download audio file

Sasa tumefikia siku ile inayoitwa “Ijumaa Kuu”, tukikumbuka tukio linalotisha, lisilotazamiwa ila wewe na mimi tutendewe jambo la ajabu mno lisilotazamiwa.

Kama tumekuwa pamoja siku hizi za maandalizi ya Ijumaa Kuu, umeshafahamu kwamba tumelenga hasa mapungufu yetu, dhambi zetu, na mwelekeo wetu kumwasi Mungu na kumwangusha Yesu aliyejitoa kipeo, aliyetoa yote kwa ajili yetu.

Labda utafikiri kwamba hayo yote yanavunja moyo, si kweli?  Ndiyo, ni kweli kabisa.  Yaani ni balaa!  Yaani giza nene la uovu unaoibuka kutoka ndani yetu, harufu mbaya ya dhambi zetu inayofika mbele zake Mungu inanuka kweli.  Lazima suluhisho na lenyewe litishe kabisa.

1 Petro 3:18  Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa.

Yule asiyedaiwa cho chote alikufa kifo cha ukatili chenye maumivu makali ili alipe deni ambalo tusingeweza kamwe kulilipa sisi.  Yaani haki haikutendeka hata kidogo tena inastaajabisha mno kuona jinsi ulivyo upendo wa Mungu kwa ajili yako na kwa ajili yangu.  Yesu aliye mwenye haki kufa kwa ajili yao wasio haki!

Na hata kama alitundikwa pale msalabani, akiishakufa, Roho wa Mungu alikuwa anatenda kazi.  Wakati dhambi zako na dhambi zangu zilisulubiwa pamoja naye, Mungu alikuwa amejiandaa kutenda jambo jipya – atuhuishe tena katika Roho.  Hii ndiyo maana ya Pasaka.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.