Waheshimu Watu Wengine
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.
Warumi 12:10 Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu.
Neno lile “kuheshimu au heshima” ni dhana ambayo tunaijua kuwa sahihi kabisa; tunafahamu kwamba ni vizuri kuheshimiana. Shida iliyopo ni kwamba, sio rahisi. Kwa hiyo, mara nyingi tunaacha kuheshimiana kwa sababu tuko bizi katika ulimwengu huu wa sasa unaoenda kasi.
Mwandishi Dale Carnegie alilelewa katika familia ya Kikristo mkoani Missouri, Marekani mwisho wa karne ya kumi na tisa. Familia yake walikuwa wakulima na kijana yule alishawishika sana na maadili ya wazazi wake, hususani wema, unyenyekevu na uadilifu wao.
Baadaye aliandika kitabu ambacho kinajulikana sana kilichopita vitabu vingine vyote kutoa ushauri katika biashara – Jinsi Kupata Marafiki na Kushawishi Watu. Je! Ni yupi asiyetaka kuwa na marafiki zaidi? Je! Ni yupi asiyetaka kuwa na uwezo wa kushawishi watu wengine? Na hata kama mimi ninatilia mashaka kidogo nia na malengo yake, bado naona ni vigumu kupinga kiini cha kitabu chake ambacho ni hiki: Wanadamu watakuwa na mwitikio mwema kwako wakati watajisikia kwamba unawaheshimu na kuwathamini na kwamba unawaelewa kwa undani.
Ujumbe wa Carnegie ni mwepesi lakini una nguvu kwa kweli: Badili jinsi unavyokaa na kuongea na watu wengine, ndipo mahusiano yako yataboreshwa pamoja na matokeo yake.
Si kwamba mtu anapaswa kuwa bingwa mkubwa wa sayansi kuelewa hilo, hapana. Lakini ni mabadiliko makubwa ambao watu wengi hawayafanyi na inakula kwao na hata kuathiri watu wengine. Mungu mwenyewe alieleza hivi:
Warumi 12:10 Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu.
Tulishachunguza sehemu ya kwanza ya mstari huu. Sehemu ya pili, kuhusu heshima, ina maana kwamba ni kama tunapaswa kushindana kuona ni nani anayeweza kuzidi wengine kuonyesha heshima kwao.
Je! Ni lini mtu aliyewahi kukuheshimu? Je! Ulijisikiaje? Kwa hiyo nauliza, Je! Mahusiano yako na wengine yangebadilikaje kama ungekusudia kuheshimu jirani zako kuliko wanavyokuheshimu, hmm?
Kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.
