Usifanye Maamuzi ya Haraka
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.
Mithali 18:15-17 Moyo wa mwenye busara hupata maarifa; na sikio la mwenye hekima hutafuta maarifa. Zawadi ya mtu humpatia nafasi; humleta mbele ya watu wakuu. Ajiteteaye kwanza huonekana kuwa ana haki; lakini jirani yake huja na kumchunguza.
Swali: Je! Unaamini kila kitu unachosoma mtandaoni?
Jibu: Wala! Lakini kwa nini watu wengi sana wanadanganywa na nadharia za njama — eti kwa sababu wameona jambo linaloendana na maoni yao?
Je! Ni mara ngapi mtu amedhalilishwa hadharani katika macho ya umma, halafu baadaye ikagundulika kwamba, baada ya uchunguzi wa kina, mtu huyo hakuwa na hatia yoyote?
Niambie, ni mara ngapi umemhukumu mtu haraka-haraka?
Alfred Dreyfus alikuwa Myahudi raia wa Ufaransa na afisa wa jeshi.
Mwaka wa 1894, alisingiziwa kuwa msaliti.
Vithibitisho vilivyotumika kumshitaki vilikuwa dhaifu kabisa, lakini jeshi, umma, na vyombo vya habari walifanya maamuzi ya haraka bila kuchunguza ukweli vizuri — walikubali tu walivyoambiwa.
Kumbe! Wakati huo huo, msaliti wa kweli aliendelea kuwa huru.
Ilichukua miaka mingi ya utafiti wa kina na sauti jasiri za watu wachache kugundua ukweli na kumwondolea Dreyfus hatia.
Lakini tayari jeraha baya lilikuwa limegusa jamii nzima ya Ufaransa.
Mithali 18:15–17
Moyo wa mwenye busara hupata maarifa; na sikio la mwenye hekima hutafuta maarifa.
Zawadi ya mtu humpatia nafasi; humleta mbele ya watu wakuu.
Ajiteteaye kwanza huonekana kuwa ana haki; lakini jirani yake huja na kumchunguza.
Sisi sote mara nyingine tunataka kuwahi kuhukumu — kukubali maoni ya watu kuwa kweli, au kujenga kiburi chetu kwa kushikilia kitu kinachoendana na mtazamo wetu kana kwamba ni ukweli kamili.
Lakini Mithali inatukumbusha kwamba,
Moyo wa mwenye busara hupata maarifa; na sikio la mwenye hekima hutafuta maarifa… Ajiteteaye kwanza huonekana kuwa ana haki; lakini jirani yake huja na kumchunguza.
Kwa hiyo, uwe mtu anayejifunza, mtu anayesikiliza wengine, na mtu anayependa kuuliza maswali sahihi.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.
