... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Unafiki na Kujidanganya

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mathayo 5:14-16 Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima. Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani. Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.

Listen to the radio broadcast of

Unafiki na Kujidanganya

Download audio file

Unafiki na kujidanganya vinaendana.  Kwa watu wanaomtazama mtu ambaye hatendi yale anayoyasema, watamwita mnafiki.  Lakini ndani yake, mara nyingi, unafiki huo unatokana na tabia yake ya kujidanganya.  Hata akijiangalia kwenye kioo, bado anabaki kipofu kwa kutokuelewa hatari yake.

Kwa mtazamo wangu, mnafiki mbaya kuliko wote ni mnafiki wa dini.  Siyo maoni yangu mimi peke yangu.  Yesu aliwashutumu vibaya manafiki wakati ule, wale viongozi wa dini.  Hata leo, si vigumu kugundua wanaojiita Wakristo lakini ni manafiki tu. 

Akiongelee swala hili la utofauti kati ya maneno na matendo, Yesu alisema hivi:

Mathayo 5:14-16  Ninyi ni nuru ya ulimwengu.  Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima.  Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani. Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.

Tusipokuwa nuru ile, wewe na mimi, tunajidanganya tu.  Usiwe mnafiki yule.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.