... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kupanga Uelekeo

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Wakorintho 4:20 Maana ufalme wa Mungu hauwi katika neno, bali katika nguvu.

Listen to the radio broadcast of

Kupanga Uelekeo


Download audio file

Najiuliza hivi, unapotathimini unatathmini afya ya familia yako kihisia na kiroho, unagundua nini? Unafurahi kwa hali yao au ni kitanzi kinachotokea machoni pako?

Tulipokuwa tunasimulia habari za familia siku hizi chache zilizopita, ni dhahiri kwamba “familia kamilifu” haipo kabisa, ni hadithi tu ambayo haina uhusiano na hali halisi ya maisha ya kila siku. 

Kila familia ina ishu zake, matatizo, migogoro, mtu anayetia aibu.  Lakini hata hivyo, Mungu anapenda familia yako kuzidi unavyoweza kueleza.  Ndio maana alimtuma Yesu kufa na kufufuka tena. Kumletea kila mmoja ndani ya familia yako, msamaha na upya wa uzima. 

Lakini, kuna kitu kimoja hapo.  Wewe na mimi tunaweza kuhudhuria kipindi cha maombi kanisani na vipindi vingine vyote, tunaweza kuwahubiria mpaka tukachoka bila kuona mabadiliko yoyote. Kuna wakati si wakati wa Mungu kutenda. Wakati mwingine unafiki wetu unachangia kwa sehemu kusababisha familia isitengamae. 

Yaani, pale mitazamo yetu na matendo yetu hayaendi sambamba na maneno yetu sisi wenyewe tutakuwa kikwazo kikubwa kuliko vyote, Mungu asiweze kuponya mahusiano ndani ya familia zetu.  Ni kwa sababu … 

1 Wakorintho 4:20  Maana ufalme wa Mungu hauwi katika neno, bali katika nguvu. 

Yesu amekusudia kukubadilisha wewe kwanza.  Yesu amekusudia kukusafisha kwanza, kukushusha na kwa kufanya hivyo, akuwezeshe kuwa balozi wake ndani ya familia yako. 

Kadiri unavyokuwa karibu na mtu, ndivyo mienendo na mitazamo yako inaleta upendo wa Kristo kwao kuliko maneno yako.  KWA HIYO, acha kusema, uanze kutenda.  Kwa sababu ufalme wa Mungu hauwi katika neno, bali katika nguvu.   

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.