... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Huzuni Uletao Mabadiliko

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

2 Wakorintho 7:9,10 Sasa nafurahi, si kwa sababu ya ninyi kuhuzunishwa, bali kwa sababu mlihuzunishwa, hata mkatubu. Maana mlihuzunishwa kwa jinsi ya Mungu, ili msipate hasara kwa tendo letu katika neno lo lote.

Listen to the radio broadcast of

Huzuni Uletao Mabadiliko


Download audio file

Huzuni si jambo ambalo tungelitamani tuwe nalo.  Hakuna sababu ya kutafuta huzuni.  Sijui ungesemaje kama ningekwambia kwamba kuna aina moja ya huzuni Mungu anataka tuwe nayo; huzuni inayo faida kwetu?

Maisha ina milima na mabonde na kinachopenda kutuangusha kabisa ni wakati mtu anatukosoa vikali; wakisuta jambo fulani ambalo tusigelipenda waseme lakini tukijua kwamba wako sahihi kabisa.  Ghafla tunagundua jinsi tulipumbazika na uharibifu tulioweza kusababisha … yaani, matokeo ya mtazamo wetu na matendo yetu.  Ni hali inayotisha kwa kweli.

Ni hali kama hiyo ambayo rafiki zake Mtume Paulo huko Korintho walihisi zaidi ya mara moja wakati aliwaandikia.  Hususani barua yake ya kwanza ambayo bado tunayeisoma, ilikuwa kali kabisa.  Lakini katika waraka wake wa pili aliandika hivi:

2 Wakorintho 7:9,10  Sasa nafurahi, si kwa sababu ya ninyi kuhuzunishwa, bali kwa sababu mlihuzunishwa, hata mkatubu.  Maana mlihuzunishwa kwa jinsi ya Mungu, ili msipate hasara kwa tendo letu katika neno lo lote.

Aina ya huzuni Mungu anatutakia, huzuni uwezayo kutusaidia sana, ni huzuni unaompelekea mtu kuamua kubadilika; ni aina ya huzuni inayotuongoza kwenye njia ya uzima wa milele.  Ni aina hii ya huzuni Mungu anaitafuta.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.