Achana na Majuto
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.
Wafilipi 3:12,13 Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! Bali nakaza mwendo ili nipate kulishika lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu. Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele; nakaza mwendo ...
Muda huu, wengi wetu tunaanza kutathmini mwaka unaoenda kuisha … Je! Uliendaje? Je! Ulikuwa mwaka mzuri au mbaya?
Vipi? Umeendaje? Ulifaulu mwaka huu? Je! Umekamilika zaidi? Umetimiza malengo yako au la? Haya yote yanagusaje hisia zako ukitafakari mwaka mpya unaokuja?
Usishangae. Kwa kweli nina maswali mengi leo, lakini nina nia njema kwa sababu Mungu yu pamoja na wewe katika maswali hayo yote. Yeye anataka ahusishwe katika mambo yajayo, ili akuongoze na nguvu zake katika mipango aliyokuandalia. Sasa, ni muda mwafaka kwetu kumwacha aongee nasi kuhusu mwaka unaoenda kwisha na jinsi tunatazamia yatakayotokea mwaka mpya.
Wafilipi 3:12,13 Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! Bali nakaza mwendo ili nipate kulishika lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu. Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele; nakaza mwendo …
Huyu ni Mtume Paulo akitathmini yaliyopita katika maisha yake na kutazama yaliyopo na kutazamia yatakayokuja. Ukweli ni kwamba hakuna aliyekamilika. Sote tunakosea. Sisi sote bado kuna mengi twapasa kujifunza. Kwa hiyo jaribu kusahau yaliyopita ili ukaze mwendo ufikie lengo ambalo Mungu ameweka mbele yako, Kwa sababu maluum
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.