... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Furaha Katika Tabu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Zaburi 119:143 Taabu na dhiki zimenipata, maagizo yako ni furaha yangu.

Listen to the radio broadcast of

Furaha Katika Tabu


Download audio file

Je! naweza kukuuliza ni yapi yanayokuletea furaha?  Kwenye kiini cha moyo wako, ni yapi yanakujaza furaha?  Halafu, furaha ile inakuaje pale mambo yanapokubadilikia na kwenda kombo? 

Kuna kitu kimoja kinaniletea furaha kubwa, ni pale mjukuu wangu, binti mwenye umri wa miaka mitatu anapokuja nyumbani kwetu, Kwa kawaida mimi niko nafanya kazi kwenye meza yangu halafu nasikia mlango unafunguka na mtoto anakimbia ndani kwenye korido huku akiniita kwa sauti kubwa  “Babuuuuuu” na kunikumbatia.  Ni furaha kweli! 

Lakini siku moja atakuwa mtu mzima. Siku moja labda hatakuwa na shangwe ya kumwona babu yake kama leo.  Na ndivyo ilivyo, hata kwa mambo bora katika ulimwengu huu wetu.

Lakini pia, kwa upande mwingine, kuna vipindi tunapitia shida na matatizo, ni basi tu. Ni kipi, kama kipo, kinaweza kukuletea furaha katikati ya kipindi kama hicho?  Hmmm?  Mtunga Zaburi aliandika hivi: 

Zaburi 119:143  Taabu na dhiki zimenipata, maagizo yako ni furaha yangu. 

Unajua, ni jambo jema kabisa kutenda mema, kufanya mapenzi ya Mungu kipindi kigumu; ukiumia kwa ndani lakini bado unaamua kuendelea kufuata wito wa Mungu juu ya maisha yako, kwa kumheshimu tu na kufuata njia zake, maagizo yake hata kama kila hatua inakuumiza. 

Unaweza kutoa machozi kama kijito lakini  bado unaskia furaha ya Bwana kuliko unavyoisikia vipindi vingine. 

Taabu na dhiki zimenipata, maagizo yako ni furaha yangu.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.