... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kitu Kinachovutia

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yohana 17:17 Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli.

Listen to the radio broadcast of

Kitu Kinachovutia


Download audio file

Yesu akitamka, ni bora tumsikilize vizuri, wewe na mimi, kwa sababu maneno yake yamejaa maana na uwezo.  Sasa maneno machache ninayotaka kukushirikisha kwayo siku ya leo, ndivyo yalivyo.

Sijui kama unamahusiano gani na Yesu leo.  Labda unaamini kwamba yeye ni Mwana wa Mungu aliyekufa na kulipa deni la dhambi zako, au labda huamini. Pengine uliwahi kumwamini lakini kwasasa unaendelea na maisha kama kawaida. Au labda wewe unajihesabu kuwa mmoja wa wanafunzi wake waliodhamiria kumtumikia. 

Mimi siwezi kujua, lakini wewe unajua na ni hakika kwamba Yesu anajua.  Samahani, nilisahau, kuna wengine wanafahamu mahali ulipo – ni Shetani mwenyewe anayetaka kukupotosha na kukupeleka mbali na Yesu kwa kutumia uongo, sio kwa kutumia uongo wa moja kwa moja (kitu ambacho utangundua haraka) bali kwa hila akitumia kweli nusu.  Anakwambia “Si unaona wewe si mtu mbaya. Wewe unaishi maisha mazuri. Hakuna sababu ya kuwa mlokole, jamani.  Endelea tu kama kawaida na utakuwa salama tu.” 

Katika dua yake ya mwisho kabla hajasulubiwa, Yesu alikusudia kuombea watu kama wewe na mimi: 

Yohana 17:17  Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli. 

Kweli, kweli yote, na kweli peke yake.  Yaani Mafundisho ya Mungu, Neno la Mungu.  Na ukweli ni kwamba, Neno lake lilikusudiwa litubadilishe.  Neno lake lilikusudiwa kubadilisha dira ya maisha yetu na mwelekeo wetu.  Neno lake lilikusudiwa kutuandaa, si kwa kuendelea kama kawaida, bali kutuandaa kwa kuhudumia kwa jina lake.  Hii ndiyo kweli kabisa. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.