... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kutafakari Kwanza

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mithali 2:1-5 Mwanangu, kama ukiyakubali maneno yangu, na kuyaweka akiba maagizo yangu; hata ukatega sikio lako kusikia hekima, ukauelekeza moyo wako upate kufahamu; naam, ukiita busara, na kupaza sauti yako upate ufahamu; ukiutafuta kama fedha, na kuutafutia kama hazina iliyositirika; ndipo utakapofahamu kumcha BWANA, na kupata kumjua Mungu.

Listen to the radio broadcast of

Kutafakari Kwanza


Download audio file

Ni ajabu namna moyo wa mtu unavyokuwa wakati mwingine, Hali halisi ya jambo fulani iko wazi machoni pake, lakini akili zake zinashindwa kupokea. Mtu anapoirudia tena mara ya pili au mara ya tatu, hapo ndipo anapoweza kuelewa. Nafikiri umeshajiuliza ni kwanini sikuelewa mwanzoni?”

ninapenda sana kuchemsha bongo kwa kutatua fumbo la maneno kwenye jedwali.  Kwa mimi ambaye kazi yangu ni kutunga maneno, na ajabu hiyo ya kutokuona kilicho dhahiri mara ya kwanza, huwa inanitokea mara tena na tena katika mchezo huo.

Mfano:  Jina la chombo kiendacho angani chenye herufi saba. Nimeshapata herufi ya tatu – P – na herufi ya tano – U – lakini…naliangaliaaaa… nikashindwa kuliona. Je!  Kuna vyombo aina ngapi vinavyoruka angani?  Baada ya nusu saa, narudi kwenye jedwali na kumbe, mara moja liko wazi kwa lugha yetu ya Kiingereza, “capsule”, yaani chombo kidogo cha kupeleka wanaanga.  Ndivyo akili zetu zinazotumika.  Mara nyingi, safari ya kwanza tunashindwa kugundua.  Ndio sababu mzee mwenye busara, Mfalme Sulemani alitamka hivi: 

Mithali 2:1-5  Mwanangu, kama ukiyakubali maneno yangu, na kuyaweka akiba maagizo yangu; hata ukatega sikio lako kusikia hekima, ukauelekeza moyo wako upate kufahamu; naam, ukiita busara, na kupaza sauti yako upate ufahamu; ukiutafuta kama fedha, na kuutafutia kama hazina iliyositirika; ndipo utakapofahamu kumcha BWANA, na kupata kumjua Mungu. 

Angalia vitenzi katika mistari hiyo: kutega sikio, kukumbuka, kusikiliza, kujitahidi, kuelewa, kuita, kupaza sauti, kutafuta, kutafutia. 

Mambo ya Mungu ni dhahiri.  Mambo ambayo yanaweza kubadilisha maisha ya mtu yako machoni pako lakini kuna wakati inabidi uyarudie tena na kuyachimba zaidi ili upate kuyaelewa vizuri. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.